Na Magesa Magesa,Arusha


MKUU wa Mkoa wa Arusha,John Mongela amewataka wakazi wa Mkoa wa Arusha hususani vijana kuchangamkia fursa ya utengenezaji wa batiki ili waweze kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umaskini.

Mongela aliyasema hayo juzi alipokuwa akizungumza na wananchi katika maazimisho ya siku rasmi ya Batiki Tanzania yaliyofanyika Mkoani hapa.

Wakati umefika kwa wananchi wa mkoani hapa hususani vijana kuchangamkia fursa hiyo ya utengenezaji wa vitu vinavyotengenezwa kwa kutumia batiki ili waweze kujiongezea kipato na kujikwamua kiuchumi”alisisitiza.

Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa kwa sasa bidhaa zinazotengenezwa na batiki zimekuwa na soko kubwa ndani na nje ya nchi hivyo kwa wale watakaojihusisha na shughuli hiyo licha ya kujiajiri wao binafsi pia watawaajiri na wengine hali itakatosaidia kukuza pato la Taifa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Roijok Progress Centre inayoratibu zoezi la kutoa elimu juu ya utengenezaji wa Batiki,Rose Urio alisema kuwa taasisi yake imekuwa ikitoa elimu juu ya utengenezaji wa batiki kwa makundi mbalimbali katika jamii.

Alisema kuwa asasi yake imezindua Samia Tanzanite Batik  Print lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa vazi la batiki linapewa kipaumbele katika jamii ambapo pia ameiomba serikali kutumia vazi hilo katika sherehe mbalimbali za kitaifa zinazofanyika hapa nchini.

“Vijana wengi sana wamekuwa wakikaaa vijiweni na kulalamika kuwa hakuna ajira hivyo wakati umefika wa kuchangamkia fursa hiyo ili waweze kujiajiri na kujiongezea kipato”alisema Urio.

Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa endapo watachangamkia fursa hiyi ya utengenezaji wa Batiki licha ya kupunguza utegemezi katika familia pia itawafanya vijana kuwa na kitu cha kufanya hali itakayowaepusha kukaa vijweni na kuweza kujiunga na makundi hatarishi.

Katika siku hiyo rasmi ya batiki Tanzania vikundi mbalimbali vya wanawake kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Arusha walijitokeza na kuonyesha shughuli zao ambapo waliipongeza asasi hiyo kwa elimu ambayo wamekuwa wakiwapatia

Share To:

Post A Comment: