UTEPE wa michauano ya Kombe la ulinzi Cup umekatwa rasmi jana kwa
mchezo mmoja kupigwa katika dimba la Magomeni ambapo timu ya Magomeni
Star dhidi Edo Combine kutoka Mwakidila zilikutana na mchezo uliamuliwa
kwa mikwaju ya Penati 4-2 baada ya dakika 90 kumalizika milango ya
timu zote mbili ikiwa migumu kufunguka
Michauano
hiyo iloliyoandaliwa na kudhaminiwa na jeshi la Polisi mkoa wa Tanga
itazikitanisha timu 20 kutoka katika mitaa mbalimbali ya jiji la Tanga
ikiwa na lengo hasa la kuhamasisha vijana kuachana na matumizi ya madawa
ya kulevya.
Akizindua
michano hiyo ya mpira wa miguu kwa vijana Kamanda wa Jeshi la Polisi
mkoa wa Tanga Henry Mwaibambe alisema michezo kwa sasa ni furaha na
ajira lakini lengo lao hasa ni kipenyeza ujumbe kwa jamii kupiga vita
matumizi ya madawa ya kulevya.
Aidha
alisema sambamba na ujumbe wa michauano hiyo kwa mwaka huu bado jeshi
hilo linaendelea kusistiza usalama wa maisha ya watu na mali zao hivyo
kuwataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano pale wanapoona Kuna
viashiria vyovyote vya uvunjifu wa amani
Michauano
hiyo itakayozihusisha timu 20 itachezwa kwa mfumo wa mtoano mpaka
bingwa apatikane kwenye fainali huku zawadi mbalimbali zikiwa zinazidi
kuvutia timu kuzidi kujipanga zaidi.
Post A Comment: