Serikali ya Tanzania imethibitisha mafanikio ya programu ya kuondoa Umaskini kwa kuwezesha wananchi wenye Uhitaji baada ya wafaidikaji kujitokeza kueleza mafanikio mbele ya Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Ndg. Ridhiwani Kikwete Katika mkutano uliofanyika katika Kitongoji cha Mwembe Baraza, kata ya Janga, Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha. 


Katika Mkutano huo wananchi mbalimbali walijitokeza kueleza jinsi mradi huo ulivyoleta mafanikio katika maisha yao, akiwemo mwananchi Ndg Hassan Korola ambaye ameeleza kuwa Bila TASAF asingesoma hadi alipofika sasa. Akieleza ushuhuda wake, Ndg Hassan alieleza kuwa programu hiyo imemsomesha toka Darasa la Kwanza hadi sasa yupo Chuo Kikuu. Ameeleza shukrani zake kwa serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa jinsi wameendelea kusaidia Watanzania wenye uhitaji.


Akiongea baada ya kupokea Taarifa mbalimbali, Ndg. Kikwete, Naibu Waziri amewashukuru wananchi kwa kukimbilia na kutumia fursa iliyopo. Amewaomba wananchi kutumia vizuri fursa hiyo kubadili maisha kama ambavyo ameshuhudia kwa makundi ya wafaidikaji. TASAF ni mkombozi kwetu tuitumie vizuri itusaidie. 

#KaziInaendelea #ZiaraPwani

Share To:

Post A Comment: