NA DENIS CHAMBI, TANGA.
MAMLAKA ya maji Safi na usafi wa Mazingira Tanga (Tanga uwasa) imekabidhi vyoo kwa shule za msingi na sekondari Funguni hii ikiwa ni sehemu ya mradi mkubwa wanaoutekeleza wilayani Pangani wa kutibu taka ngumu uliogawanywa katika sehemu kuu tatu za ujenzi wa miundombinu ya kupokea na kutibu taka ngumu uliopo mbioni kukamilika ukifikia 92%, ujenzi wa vyoo katika maeneo matatu ya shule ya msingi na sekondari Funguni iliyokwisha kukamilika kwa 100% pamoja na eneo la kituo kikuu cha mabasi uliofikia 98% hii ikilenga hasa kuwakinga na magonjwa ya mlipuko wananchi wanaozunguka maeneo hayo.
Miradi
hiyo inayotekelezwa na Mkandarasi M/S PERNTELS COMPANY. Ltd kwa gharama
ya shilingi Billion moja ambazo ni ufadhili wa serikali na inatarajiwa
kukamilika na kukabidhiwa Septemba, 2023.
Akitoa
taarifa ya utekelezaji wa miradi hiyo mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya
maji Safi na usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly
amesema kuwa miradi hiyo inatekelezwa kupitia ufadhili wa serikali
ambapo kupitia mbunge wa Jimbo la Pangani na waziri wa maji Jumaa Aweso
kiasi cha shilingi Billion moja kilitolewa kwaajili ya kutekeleza mradi
huo.
"Katika mradi huu
tumelenga kwaajili ya kutoa maji ambayo baada ya kuyatibu yawe ni maji
safi na salama Tanga Uwasa imetekeleza mradi huu kwa lengo la kuboresha
huduma kwa wakazi wa mji wa Pangani na nje ya Pangani kwa ujumla na
mradi huu umejengwa kwa ufadhili wa serikali kwa gharama ya shilingi
billion moja utekelezaji na gharama baada ya kupata bajeti na kufanya
mchakato wa ununuzi mradi ilipatikana kwa shilingi million 998 na lengo
la mradi kwa ujumla wake ni kukamilika September 30,2023." alisema
Mhandishi Hilly.
"Kazi
zilizotegemewa na ambazo zimefanyika kulikuwa na ujenzi wa mtambo wa
kuchuja maji taka ambao umefikia 92%, kujenga vyoo vitatu eneo la shule
ya msingi na sekondari Funguni na kituo cha mabasi, pia kulikuwa na
utaratibu wa kupata gari la kunyonya maji taka na tayari lipo tayari
litakuja kwaajili ya makabidhiano lakini pia tulihakikisha kuwa
waliotupa maeneo ya mradi wamepata stahiki zao" aliongeza .
Akikabidhi
moja ya mradi wa choo katika shule ya msingi Funguni tayari kwa
kuanza kutumika mkuu wa wilaya ya Pangani Zainab Abdallah aliwapongeza
Tanga Uwasa kwa kuendelea kufanya huduma zake na kuwafikia wananchi
karibu sambamba na kujali afya zao kwa kujenga vyoo katika maeneo
yanayowazunguka.
"Kwa
niaba ya serikali tunawashukuru sana Tanga Uwasa kwa kazi kubwa
wanayofanya katika kuhudumia wananchi wa Pangani , tunaona mradi huu wa
kuhakikisha maji taka yanaweza kudhibitiwa nimpongeze sana mbunge kwa
kuhakikisha fedha hizi zinapatikana lakini pia wamefikia jamii kwa
kujenga vyoo katika shule yetu ya msingi na sekondari Funguni lakini na
stendi tunawapongeza sana" alisema Zainab.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa chama cha mapinduzi 'CCM' wilaya ya Pangani
Abdallah akiwa katika ziara ya kamati ya siasa kukagua miradi ya
maendeleo pamoja na kuongea na wananchi amewapongeza Tanga Uwasa kwa
kutekeleza miradi hiyo.
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Pangani Abdallah Mahmoud akikata utepe kuashiria uzinduzi wa vyoo kwajili ya wanafunzi vilivyojengwa na mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Tanga uwasa katika shule za msingi na sekondari Funguni wilayani humo.
Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainab Abdallah akizungumza mara baada ya uzinduzi wa vyoo vya shule ya msingi na sekondari Funguni vilivyojengwa na mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira Tanga Uwasa
Post A Comment: