Na Denis Chambi, Tanga
Wanafunzi
, walimu pamoja na waumini wa dini ya Kiislamu zaidi ya 130 kutoka
Taasisi ya Bilal Muslim Mission of Tanzania tawi la Tanga wameshiriki
kikamilifu katika zoezi la uchangiaji wa damu salama katika hospotal ya
rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo ikiwa ni maadhimisho ya mwaka mpya wa
kiislamu ukiambatana na kukumbuka kifo cha mjukuu wa Mtume (S. A .W)
Imamu Houssein Ally.
Akizungumza
mara baada ya tukio hilo Mkuu wa shule ya wasichana katika taasisi hiyo
Sheikh Sajad Hassan amesema kuwa uchangiaji wa damu katika hospitali
hiyo kawaida yao ya kila mwaka ikiwa ni ishara ya kuonesha moyo wa
kujitolea wahitaji mbalimbali hususani watoto na mama wajawazito
waliopo hospital wanaohitaji kuongezewa damu.
"Lengo
la kuja kuchangia damu hapa hospital ni kujitolea sadaka,
tunaifungamanisha sadaka yetu na tukio la kuwawa kwa mjukuu wa bwana
mtume (S.A .W) Hussein Bin Allyy aliyeuwawa mwaka 61 Hijiria huko Irak
aliyekuwa wakiipigania dini kwa lengo la kukemea mabaya na kuamrisha
mema, aliyetoka kutetea wanyonge na wale waliodhurumiwa"
"Na
sisi taasisi ya Al Bilal Muslim hili ni zoezi ambalo tunalifanya kila
mwaka tukija kuchangia damu katika maeneo tofauti tofauti lengo na sisi
ni kuonyesha kwamba tumesimama pamoja na mjukuu wa bwana mtume (S.A.W)
katika kutetea wanyonge, damu itasaidia wanyonge, pia tunasimama na
kukemea dhuruma zozote zinazoendelea ulimwenguni" alisema Sheikh
Hassan.
Kwa upande wake
mkuu wa idara ya maabara ya damu katika hospital ya rufaa ya mkoa wa
Tanga Bombo , Sinde Ntobu ameishukuru na kuipongeza taaisisi hiyo kwa
kuona kuwa wanayo nafasi kubwa kuokoa maisha ya watu wanaofika
hospitalini hapo kupatiwa huduma ikiwemo kuongezewa damu.
Alisema
uhitaji wa damu kwa mwezi katika hospital hiyo ni mkubwa tofauti na ile
inayochangiwa ambapo uhitaji wao unafikia lita 500 hadi 600 wakiwa na
upungufu wa damu kwa Unit 250 hadi 300 hivyo kuziomba taasisi na watu
binafsi kuona umuhimu wa kuchangia damu ili kuokoa maisha ya watu.
"Tunashukuru
sana siku ya leo tupo na wenzetu wa taasisi ya Bilal Muslim ambao kila
mwaka huwa wanakuja kuchangia damu salama kwaajili ya wagonjwa wenye
uhitaji wa damu tunawashukuru sana kwasababu kila mwaka wana tukio kama
hili tunawapongeza kwa moyo wao huo wa kuweka katika kalenda yao"
alisema Ntobu.
" Sisi
kama hospital kwa wastani kwa mwezi tunatumia chupa za damu 500 mpaka
600 lakini uwezo wa kuchangia damu ambayo inapatikana mara nyingi
tunapata unit 250 mpaka 300 kwahiyo uhitaji wa damu kwa wagonjwa ni
mkubwa , kikubwa niiase jamii kwa sababu damu ni huduma ambayo
hainunuliwi mahali popote bali inatoka kwa wananchi kwenye jamii
tunahitaji jamii ijitolee damu kwa hiari lakini muamko wa jamii katika
zoezi hili ni mdogo" alisisitiza.
Mbali
na uchangiaji wa damu taasisi ya Al Bilal Musilim Mission of Tanzania
pia iliweza kuchangia vitu mbalimbali ambavyo ni mahitaji kwa wakinamama
wanaojifungua katika hospital hiyo.
Mkuu wa shule ya wasichana wa taasisi ya Bilal Muslim Mission of Tanzania tawi la Tanga ,
Sheikh Sajad Hassan akishiriki katika zoezi la uchangiaji wa damu salama lililofanyika july 27 katika hospital ya rufaa ya mkoa wa Tanga Bombo.
Damu salama iliyokwisha kuchangiwa na walimu , wanafunzi na waumini wa dini ya kiislamu kutoka katika taasisi ya Bilal Muslim Mission of Tanzania tawi la Tanga ,
Sheikh Sajad Hassan akishiriki katika zoezi la uchangiaji wa damu
salama lililofanyika july 27 katika hospital ya rufaa ya mkoa wa Tanga
Bombo.
Baadhi ya vitu mbalimbali ikiwemo sabuni vilivyotolewa kwa wazazi waliopo katika hospital ya rufaa ya mkoa wa Tanga Bombo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho yanayofanywa kila mwaka na taasisi ya Bilal Muslim Mission of Tanzania tawi la Tanga.
Post A Comment: