Na Chalila Kubuda,
SERIKALI imesema katika mapinduzi ya sekta ya elimu inakwenda kuwekeza kwenye ujuzi hali itakayosadia kuleta maendeleleo katika nyanja mbalimbali.
Katika kupata elimu ya ujuzi Serikali imeanzisha mahusiano kati ya Vyuo vya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi vya nchini na Vyuo vya Ufundi nchini China ili kuweza kuzalisha vijana wenye ujuzi huo.
Hayo ameyasema Waziri Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda wakati akifungua Semina ya Vyuo vyuo vya Ufundi Stadi kati ya Tanzania na China iliyofanyika Kibaha mkoani Pwani.
Amesema ushirikiano wa sasa ni wanafunzi wanaosoma vyuo ufundi stadi kwenda kujifunza nchini China ambapo Tanzania wameenda 30 ambao idadi hiyo inatakiwa kuongezeka kutokana mahitaji yaliyopo ya vijana kupata ujuzi.
Amesema Tanzania kuna kazi kubwa ya kujifunza nchini China kutokana hatua waliyopiga kwenye sekta mbalimbali.
Profesa Mkenda amesema kuwa Chuo cha DIT wanafunzi wa uhandisi na Teknolojia watasoma mwaka moja na miaka miwili watasoma nchini China na wataporudi watamalizia mwaka mmoja na kupata shahada ya kwanza ambapo atakuwa na Diploma ya ujunzi kutoka China.
Amesema kuwa katika mkutano huo vyuo vya ufundi stadi zaidi ya 30 kutoka nchini China vimeshiriki ambapo ni matunda ya Tanzania kwa vijana waliopo katika vyuo vya ufundi kwenda kusoma na kupata ujuzi.
"Tunakwenda kwa kasi zaidi katika kuwa na wataalam wenye ujuzi wenye kuzalisha na kujenga uchumi wa kuongeza pato la taifa linalotokana na nguvu kazi watalaam katika maeneo mbalimbali"amesema Profesa Mkenda.
Amesema kuwa wamekubaliana na Kampuni ya Group Six wanafunzi watasoma katika vyuo vya China watafanya mafunzo ya vitendo kazi na kampuni hiyo na watamohitimu wanaweza kufanya nao kazi wamekwenda kusoma
Nae Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) Dkt.Adolf Rutayuga malengo ni ushirikiano katika utoaji wa mafunzo kutokana nchi hiyo kuwa Teknolojia ya ujuzi.
Amesema nia hiyo kwa Tanzania ni kutaka vijana kuwa na ujuzi na kuweza kutumika maeneo mbalimbali na kuleta tija.
Amesema vyuo vya ufundi nchini China wanafunzi wake wanashiriki katika kutengeneza bidhaa ambazo zinaingia sokoni na kupata soko.
Dkt.Rutayuga amesema Vyuo vya Ufundi vilivyoshiriki kutoka nchini China ni 30 na vyuo vya Tanzania 40 ambao watakutana na kutengeneza daraja la ushirikiano.
Amesema kuwa vijana wanaosoma vyuo vya kati nchini China ndio chachu ya maendeleo hivyo Tanzania inakwenda katika mfumo wa wa nchi hiyo katika kutoa ujuzi kupitia vyuo vya mafunzo ya ufundi Stadi.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) Dkt.Adolf Rutayuga akizungumza kuhusiana na mafanikio ya semina hiyo kwa Tanzania kupata ujuzi kutoka katika vyuo vya ufundi nchini China katika Semina iliyofanyika Kibaha mkoani Pwani.
Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri NACTVET Profesa John Kondoro akizungumza kuhusiana na mafanikio yatayopatikana kutokana na vijana kupata ujuzi nchini China katika Semina kati vyuo vya ufundi vya China na Tanzania iliyofanyika Kibaha mkoani Pwani.
Picha ya Mgeni Rasmi Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda na Meza Kuu pamoja na wawakilishi wa vyuo 30 ufundi Stadi vya China katika semina katika vyuo vya ufundi vya Tanzania na China.
Picha ya Mgeni Rasmi Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda na Meza Kuu pamoja na Kamati ya Maandalizi ya Semina kati ya Vyuo vya Ufundi Stadi vya Tanzania na China.
Picha ya Mgeni Rasmi Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda na Meza Kuu pamoja na Wakuu wa Vyuo na Taasisi kwenye Semina kati ya Vyuo vya Ufundi Stadi vya Tanzania na China.
Post A Comment: