SERIKALI ya Awamu ya Sita kupitia Wizara ya Madini imesema sekta ya madini imepewa msukumo mkubwa kwenye sekta hiyo sambamba na kuhakikisha inaondoa changamoto ambazo zinawakabili wachimbaji madini.
Akizungumza katika mkutano wa wwchimbaji madini uliofanyika leo jijini Dar es Salaam Waziri wa Madini Dotto Biteko ameeleza wamekutana kwa ajili ya kujadili changamoto lakini wakati huo huo kuelesa Serikali inafanya katika sekta ya uchimbaji madiji ili wachimbaji wafanye shughuli zao kwa ufanisi.
Hivyo kupitia mkutano huo ulioandaliwa na Chama Cha Wachimba Madini Tanzania Biteko miongoni mwa maeneo ambayo yataangaliwa ni miundombinu ya umeme pamoja na barabara kwa kuhakikisha maeneo ya migodi yanaboreshwa.
Pamoja na hayo amesema Serikali imeweka msumkumo mkubwa kwenye miundombinu ya uzalishaji ,hivyo katika fedha zote zilizotengwa kwa ajili ya umeme vijijini na mahali pengine karibu asilimia 20 ya fedha hizo zimekwenda maeneo ya migodi ya wachimbaji wakubwa,wakati na wadogo
"Wizara ya Madini inatoa shukrani kwa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwani amefanya mambo makubwa katika sekta ya madini na maeneo mengi ya uchimbaji yanapelekewa umeme, " ameseema.
Aidha amesema katika kutatua maeneo ambayo yamekuwa na muingiliano wa migodi na uchimbaji, tayari Rais Dk.Samia ametoa maelekezo Wizara hiyo kukaa na Wizara ya Maliasili na Utalii kupata ufumbuzi wake na hilo litatekelezwa haraka.
"Tunafahamu changamoto wanazokumbana nazo wachimbaji wetu maeneo ya hifadhi lakini lazima tukubali tunaowajibu kulinda na kuhifadhi mazingira lakini eneo lenye leseni lazima uchimbaji ufanyike kwa kufuata sheria na taratibu zilizopo."
Awali Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji Madini Tanzania Mhandisi Filbert Rweyemamu amesema ili wafanye kazi zao ufanisi ni lazima kuwepo kwa mahusiano mazuri kati ya Mkusanyiko wa hiari wa watafiti,wachimbaji na watoa huduma katika sekta ya Madini.
Amesema kupitia mikutano hiyo ukiwemo wa leo wametoa taarifa muhimu za maendeleo ya shughuli zao pamoja na kuieleza Serikali mambo yanaweza kurahisisha shughuli zao.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tembo Nickel Benedick Masunzu amesema katika Mradi wao wa uchimbaji wa Madini aina ya Nickel fedha ni muhimu zaidi na tayari kampuni hiyo imefanikiwa kupata kiasi cha fedha kitakachosaidia kuanza uzalishaji wa madini hayo ifikapo mwaka 2026.
Wakati huo huo Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Faru Ghraphite inayotarajia kuchimba madini hayo kwenye mgodi wa Mahenge mkoani Morogoro Alimiya Othman amesma Wizara ya Fedha na Benki Kuu ya Tanzania( BOT) wameweza kutafuta suluhisho kutatua changamoto za kifedha kwa kuwa wao ni wadau wakubwa
Post A Comment: