Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema kuwa serikali inafanyika kazi malalamiko yote yanayotolewa na wananchi juu ya huduma za mawasiliano nchini.
Aidha miongoni mwa mipango itakayotekelezaa mwaka huu muda wowote kuanzia sasa ni kurusha satelite ya Tanzania kwaajili ya mawasiliano.
Akifungua kikao kazi cha siku tatu cha viongozi wa wizara na taasisi zilizochini ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Waziri Nape alisisitiza mshikamano upendo ili
Alisema watanzania wanastahili huduma bora za mawasiliano na rahisi zinazopatikana kila mahali ingawa bado kunamalalamiko ya watanzania juu ya huduma za mawasiliano nchini.
Alisema mwaka huu Tanzania imeahidi kurusha satelite yake na kusisitiza wakati wowote satelite hiyo itarushwa
"Tulipokwama,tuliposuasua tutafanya tathimini ya kina na kuambiana hali ilivyo ikiwemo kufanya maboresho ili mwaka huu wa fedha 2023/24 tuweze kuendelea mbele"
Alimshukuru Rais Samia Hassan Suluhu kwa kwamuda anaoutoa katika maboresho mbalimbali ya Wizara ya habari sanjari na kuhudhuria shughuli mbalimbali zinazofanyika.
Alisema wizara imepitia sheria,sera ikiwemo mapitio ya sheria mpya ikiwemo kanuni zinazosimamia mambo mbalimbali ya habari
"Tulipofanikiwa ni vizuri kupongezana na tutaagalia tuliyojipangia mwaka huu wa fedha yapo mambo mbalimbali lakini naamini tunaweza na tutafanikiwa,tushikamane zaidi"
Naye Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Mohamed Khamis Abdulla alisema wizara hiyo imepata mafaniko mbalimbali kwasababu ya upendo,umoja na amani walionao viongozi na watumishi kwa ujumla , na kutoa rai kwa viongozi wa taasisi mbalimbali za serikali waliopo chini ya Wizara hiyo kutumia nafasi zao za kimamlaka kwa kuwaelekeza kazi wafanyakazi wa chini ili nao wajitume zaidi
"Watumishi tukiwa na umoja na kujituma ni nguzo muhimu katika Utekelezaji wa majukumu yetu na ninaomba tufanye kazi kwakujitima na si kushurutishwa kwasababu hakuna haki bila wajibu"
Vilevile aliwaagiza wakuu wa taasisi kusimamia Utekelezaji wa sera, kanuni,miongozo taratibu zinazohusu haki na utawala bora .
Alisisitiza viongozi hao wasimamie stahiki za wafanyakazi ikiwemo utawala bora ikiwemo kuacha alama katika taasisi zilizopo
Ambapo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar,Shomari Omari Shomari alishukuru wizara hizo mbili za Zanzibar na Tanzania Bara kushirikiana kwa pamoja na kuahidi kuimarisha ushirikiano huo katika kuondoa kero za muungano ikiwemo kuongeza uchumi wa kidigitali.
Aliongeza kuwa kwaupande wa Zanzibar wanaimarisha wanauchumi wa bluu lakini pia uchumi wa kidigitali nao ni muhimu katika ukuzaji wa sekta mbalimbali
Katika kikao hicho mada mbalimbali zitatolewa zikiwemo mawasiliano ndani ya taasisi,Tanzania ya Kidigitali, Mabadiliko ya Sera ya Tehama, Mpango Kazi wa shughuli za kazi,maadili ya utumishi wa umma, utunzaji wa kumbukumbu na nyaraka sanjari na usalama na utunzaji wa siri za kikazi.
Lakini pia viongozi wa taasisi hizo walipewa vitendea kazi kwaajili ya uboreshaji wa shughuli zao za kazi
Post A Comment: