SENYAMULE- CHEMBA BILA HOJA INAWEZEKANA
Na: Elizabeth Paulo, Dodoma
Mkuu wa Mkoa Wa Dodoma Mheshimiwa Rosemary Senyamule ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Chemba kwa kua na mfululizo wa Hati safi kufuati taarifa ya Mkaguzi wa Hesabu za serikali zilizoishia Juni 30, 2022.
Senyamule ametoa pongezi hizo Jana tarehe 13 Julai 2023 Alipokua Wilayani hapo katika mfululizo wa vikao maalumu vya Baraza la Madiwani kwa lengo la kujadili hoja za Mkaguzi Mkuu wa Serikali kwa hesabu zilizoishia tarehe 30 Juni, 2022.
Amesema ili Halmashauri ya Wilaya ya Chemba iendelee kupata Hati Safi katika kaguzi zote kila mwaka kama ambavyo umekuwa ni utamaduni wa Halmashauri hiyo ni vema kudumisha ushirikiano chanya baina ya Waheshimiwa Madiwani, Watendaji wa Halmashauri, Viongozi na Wadau mbalimbali wa Halmashauri.
"Halmashauri ya Wilaya ya Chemba ilikuwa na hoja 50 ambazo zimegawanyika katika sehemu tatu, hoja za mwaka jana 25, hoja za miaka iliyopita 25 na agizo la LAAC ambalo ni moja" ameeleza Mhe.Senyamule
Aidha, amesema kati ya hoja 50, 13 zimefungwa na 37 bado zipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji chini ya Menejimenti ya Halmashauri chini ya usimamizi wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo.
”Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Chemba chini ya usimamizi wa Baraza la Madiwani inapaswa kuweka mkazo mkubwa kujibu hoja zote badala ya hoja za hivi karibuni ” Senyamule amesisitiza.
Amesema ili kuondokana na changamoto ya Halmashauri kuwa na hoja nyingi zisizofanyiwa kazi ameagiza Kamati ya Fedha ambayo inakutana kila mwezi kuwa na agenda ya kudumu ya kujadili mwenendo wa ujibuji wa hoja za ukaguzi za Mkaguzi wa Ndani wa Halmashauri na zile zinazotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na kuchukua hatua stahiki pale inapobainika kuwa Menejimenti imefanya uzembe katika kufanyia kazi hoja za ukaguzi.
“Kuna uzembe wa watu kutomaliza hoja kwa Makusudi watumishi jipangeni tunapokuta mtu anachelesha kuweka Viambatanisho kuna kitu hakiko sawa hapo naamini mkiweka mkakati wa pamoja hoja zote zitafutwa na Chemba bila hoja inawezekana endapo mtatumia ipasavyo vikao vya kamati ya Ukaguzi” Senyamule amesisitiza.
Aidha, Senyamule ametoa msisitizo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba kuimarisha ukusanyaji wa mapato walau kufikisha Bilioni 2 kwa kufanya ubunifu mbalimbali wa vyanzo vya mapato.
Kupitia kikao hicho maalumu cha Baraza la Madiwani Senyamule pia ametumia hadhara hiyo kusisitiza suala la elimu, mazingira na kilimo na kuagiza kuwa ni agenda ya kudumu katika vikao ngazi zote.
“Elimu ni agenda ya kudumu, ni lazima watoto waende shule na msaidie Kutokomeza utoro na tuwape elimu wazazi ili waweze kusaidia katika kutokomeza suala na utoro ma shuleni.
Awali Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Bw. Ally Gugu amewaasa Watumishi kuendeleza kushirikiana na Utawala vizuri ili kurahisisha utendaji na kufuata Sheria, taratibu, kanuni za utumishi wa umma bila kupoteza muda katika utendaji
Naye Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mheshimiwa Gerard Mongela ameushukuru Uongozi wa Mkoa hususani Mkuu wa Mkoa kwa Miongozo na maelekezo anayowapatia na kusema hatua waliyofikia ni kutokana na Maelekezo ya uongozi wa mkoa.
Akizungumza kwa niaba ya Madiwani Mh Mweshimiwa Rajabu Diwani Kata ya Babayu amesema watahakikisha kudumisha ushirikiano wao na watumishi wengine katika kutekeleza majukumu Yao huku amekiri kwa kusema kikao hicho kimekua kifupi sana kutokana mwenendo mzuri wa Halmashauri ya wilaya hiyo.
Akifunga kikao hicho Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chemba Mheshimiwa Said Sambala amesema Kama watumishi watahakikisha Yale yote yaliyozungumzwa yanatekelezwa kwa Vitendo.
Post A Comment: