Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Mwenge wa uhuru umewasili Mkoani Shinyanga leo Alhamisi Julai 27,2023 ambapo umepokelewa katika Shule ya Msingi Buganika Wilayani Kishapu ukitokea Mkoani Simiyu.
Mwenge wa uhuru utakimbizwa umbali wa kilomita 571.5 na kuona, kuweka mawe ya msingi, kufungua na kuzindua jumla ya miradi 41 yenye thamani ya shilingi bilioni 14.27 katika Mkoa wa Shinyanga.
Miradi 11 yenye thamani ya shilingi bilioni 7.8 itawekewa mawe ya msingi, miradi 14 yenye thamani ya shilingi bilioni 3.3 itazinduliwa, miradi 4 yenye thamani ya shilingi bilioni 1.3 itafunguliwa huku miradi 12 yenye thamani ya shilingi bilioni bilioni 1.5 itaonwa.
Mwenge wa uhuru kwa mwaka 2023 unaendelea kukimbizwa katika mikoa mbalimbali Nchini ukiongozwa na Bwana Abdalla Shaim Kaimu pamoja na kaulimbiu inayosema tunza mazingira, okoa vyanzo vya maji kwa ustawi wa viumbe hai na uchumi wa Taifa.
Post A Comment: