Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba akitoa taarifa ya utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida kwa kipindi cha Januari 2023 hadi Juni 2023 katika mkutano uliofanyika Ukumbi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Singida, kwa Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Singida leo Julai 28, 2023.


Na Dotto Mwaibale, Singida

PATO la Mkoa wa Singida (GDP) limekuwa kutoka Sh. Trilioni 2.8 mwaka 2020hadi kufikia Sh.Trilioni 3.019 kwa mwaka 2021.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba Julai 28, 2023 wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida kwa kipindi cha Januari 2023 hadi Juni 2023 katika mkutano uliofanyika Ukumbi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Singida, kwa Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Singida.

Taarifa hiyo imekuja baada ya Kamati ya Siasa Mkoa wa Singida kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika halmashauri zote saba ambazo ni Ikungi, Mkalama, Manyoni, Wilaya ya Singida, Iramba, Itigi na Manispaa ya Singida.

Akizungumzia  mpango wa bajeti ya mkoa imeongezeka kutoka Sh.199,170,767,000 mwaka 2021/2022 hadi kufikia Sh.230,988,225,000 amabapo mkoa umekadiria kutumia kwa mwaka 2023/2024.

Serukamba alisema pato la wastani la kila mtu kwa Mkoa wa Singida limekuwa kutoka Sh.1,651,785 kwa mwaka 2020 hadi kufikia Sh.1,721,195 mwaka 2021.

Akizungumzia bajeti ya Mwaka 2022/ 2023 katika mwaka wa fedha wa 2022/2023 Sekretarieti ya Mkoa na Halmashauri ziliidhinishiwa bajeti ya jumla ya Sh.239,808,971,000 ambapokati ya fedha hizo Sh.134,538,706,000 ni kwa ajili ya mishahara, Sh.21,337,548,000 kwa ajili ya matumizi mengineyo na Sh.83,932,717,000 kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

"Hadi kufikia Juni 30,2023 Mkoawetu ulipokea Sh.218,212,991.409.84 sawa na asilimia 91 ambapo mishahara ni Sh.118,655,587,060 sawa na asilimia 88.1, matumizi mengineyo 22,263,611,331.34 sawa na asilimia 104.3 na maendeleo Sh.77,293,793,018.5 sawa na asilimia 92.

Alisema kwa upande wa bajeti ya Taasisi, katika mwaka wa fedha 2022/2023 zilikisia kutumia Sh.68,771,671,207 ambapo hadi kufikia Juni 30,2023 zilipokea Sh.63,751,112,207 sawa na asilimia 92.6.

Baada ya mkuu wa mkoa kuwasilisha taarifa hiyo wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Singida waliipitisha na kuijadili.

Serukamba alitumia nafasi hiyo kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo Mkoa wa Singida.

Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dk.Fatma Mganga, akizungumza kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  Mkoa wa Singida, Martha Mlata, akizungumza kwenye mkutano huo. 
Katibu wa CCM Mkoa wa Singida, Lucy Boniface, akiongoza mkutano huo.
Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Singida wakiwa kwenye mkutano huo.
Wabunge wa Mkoa wa Singida wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida, Yagi Kiaratu (wa pili kutoka kushoto) akiwa na viongozi wengine kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Wenyeviti  wa Halmashauri za Wilaya wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Uwasilishaji wa taarifa na mkuu wa mkoa ukiendelea.
Taswira ya mkutano huo. 

Share To:

dotto mwaibale

Post A Comment: