Na Dotto Mwaibale, Manyoni
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida,Martha Mlata
ameiagiza Halmashauri ya Itigi Wilaya ya Manyoni kupeleka madawati katika Shule
Mpya ya Sekondari ya Mwamagembe kabla ya Agosti 15, 2023 ili wanafunzi waanze
masomo.
Mlata ametoa agizo hilo leo Julai 29, 2023 wakati alipokuwa katika ziara ya
kikazi ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo na kufanya mkutano wa
hadhara ambapo alipokea kero mbalimbali za wananchi wa Kata hiyo..
"Niseisikia taarifa yenu kuwa wanafunzi wa kata hii wanalazimika
kutembelea kilomita 70 kwenda Rungwa kwa ajili ya kusoma jambo hili
haliwezekani kwani linawatesa watoto nakuagiza Mwenyekiti wa Halmashauri ya
Itigi hakikisheni kabla ya Agosti 15, 2023 muwe mmeleta madawati hapa shuleni
wanafunzi waanze masomo," alisema Mlata.
Aidha Mlata alimwagiza Afisa Tarafa wa Itigi, Eliutha Augustone kuwasiliana
na Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Kemirembe Lwota ili awasiliane na viongozi wa
idara ya elimu wafanye uteuzi wa Mkuu wa Shule hiyo kuhakikisha anamteua Mkuu
wa Shule hiyo.
Mlata alisema alichobaini ukanda huu wa Kata za Mawamagembe zimesauliwa
sana kielimu na kuagiza nguvu zaidi ziwekezwe ili kuhakikisha watoto wanapata
elimu kama ilivyo kata zingine.
Diwani wa Kata hiyo, Jonathan Dulle akielezea changamoto ya shule hiyo kutoanza
kutumumika kutokana na sababu mbalimbali na kwamba mwaka jana wanafunzi
waliofaulu na kuanza masomo katika Shule ya Sekondari ya Rungwa walikuwa 96
wanaoendelea na masomo ni sita na waliohama ni 46 na kuwa wanafunzi 44
hawajulikani walipo.
Mlata baada ya kukagua ujenzi wa shule hiyo alifanya mkutano wa hadhara na kuzungumza na wananchi wa kata hiyo ambapo alitumia nafasi hiyo kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi zilizotekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC) Yohana Msita, akizungumza kwenye mkutano huo.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Singida, Elphas Lwanji akizungumza kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida,Martha Mlata, akipokelewa na viongozi mbalimbali wakati wa ziara hiyo.
Post A Comment: