Mwenge wa Uhuru Umejiridhisha na kukagua Miradi mbalimbali ya Maendeleo Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro Mkoani Arusha.

 Awali akitolea ufafanuzi juu ya miradi iliyokaguliwa pamoja na Gharama zake Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Mwalimu Raymond Mwangwala Amesema jumla ya Miradi ni 9 yenye Gharama zaidi ya Billioni Moja.

Baada ya ufafanuzi huo , Kiongozi wa Mbio za Mwenge Abdala Shaibu Kaimu akitoa ujumbe wa Mwenge Amesisitiza kupiga vita Matumizi ya Dawa za kulevya, Na kumtaka DC Mwangwala Pamoja na Ofisi ya Takukuru, kufanya uchunguzi wa Vifaa tiba katika kituo Cha Afya Cha Sukenya kilichozinduliwa Leo.

 Kwa Upande wa Elimu Shule ya Msingi Monic kata ya ngaresero Mbunge wa Jimbo Hilo Emmanuel Shangai amesema ujenzi wa Madara umetokana na fedha za Boost kutoka Serikalini 

Sambamba na Hilo Mwenge wa Uhuru ulifika pia katika Daraja la Sale na kufanya Ukaguzi Ambapo wananchi wamesema wamekuwa wakiwapoteza Ndugu zao kipindi Cha Masika , huku utunzaji wa Mazingira ukisisitizwa ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.



Share To:

Post A Comment: