JUMLA ya MIRADI 14 yenye thamani ya bilioni 1.8 wilayani Monduli Mkoani Arusha, imezinduliwa ,kuwekwa mawe ya msingi na kutembelewa na mbio za mwenge wa uhuru kitaifa ukiwemo mradi wa maji wa sh,milioni 500.7 katika kata ya Meserani.
Mkuu wa wilaya ya Monduli,Joshua Nasari alieleza hayo wakati akikabidhiwa mwenge wa uhuru katika eneo la Meserani ,ukitokea jijini Arusha, ambapo alisema kuwa miradi hiyo inatekelezwa na fedha kutoka serikali kuu,Halmashauri na nguvu za wananchi.
Alifafanua kuwa miongoni mwa fedha hizo kiasi cha sh,bilioni 1.17 ni kutoka serikali kuu sh,milioni 30 kutoka halmashauri na nguvu za wananchi sh,milioni 600.
Akizindua mradi wa maji katika kijiji cha Meserani Bwawani, kata ya Meserani , wenye thamani ya sh,milioni549,780,722 utakao hudumia wakazi wapatao 4752,kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa,Abdalah Shaib Kaim alipongeza mradi huo kwa kukidhi ubora na matumizi sahihi ya fedha za umma yanayoendana na thamani ya mradi na kusisitiza kuwa lazima utekelezaji wa miradi uzingatie uzalendo wa kweli.
“Ndugu zangu wana Monduli niwapongeze sana kwa mradi huu mkubwa kwani umezingatia ubora, vigezo vyote vinavyotakiwa ikiwemo nyaraka sahihi za mradi ,nyinyi ni wazalendo wa kweli”
Naye meneja wa mamlaka ya maji Monduli, RUWASA, ,mhandisi Neville Msaki ,alisema mradi huo pia utahudumia vijiji jirani vya Engorika,Lengiloriti na Moita Kiloriti na unatekelezwa na fedha kutoka serikali kuu .
Naye mbunge wa Monduli, Fredrick Lowasa, amepongeza Rais Samia suluhu Hassan kwa kupeleka fedha katika Jimbo la Monduli zilizofanikisha kutekelezwa kwa miradi mingi ya maendeleo ukiwemo mradi mkubwa wa maji ambayo imezinduliwa na mbio za mwenge.
Alisema rais samia aliahidi kutoa fedha kiasi cha sh,bilioni 16 kwa ajili ya kutatua changamoto ya maji kutoka Ngaramtoni wilaya ya Arumeru, utakaohudumia vijiji 13 na hivyi kuondoa changamoto ya maji kwa kiasi kikubwa katika jimbo hilo.
“Namshukuru rais samia kwa kuendelea kutoa fedha za miradi ya maendeleo jimbo la monduli ”
Mwenge wa uhuru, pia umezindua miradi mbalimbali ya Zahanati,Madarasa,vikundi vya vijana,barabara ya Lami,chanzo cha maji na klabu ya kikundi cha vijana wapinga rushwa wapatao 50 katika chuo cha maendeleo ya jamii Monduli .
Post A Comment: