Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Bwana Abdalla Shaim Kaim amepongeza juhudi zilizofanyika katika ukamilishaji wa miradi ya maendeleo kwa kiwango chenye ubora katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.

Ametoa pongezi hizo leo Ijumaa Julai 28,2023 baada ya kutembelea na kuona miradi mbalimbali ya Maendeleo katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga baada ya kukamilisha mbio zake Wilayani kishapu.

Kiongozi huyo wa Mbio za Mwenge wa uhuru Taifa amekagua nyaraka zote na kujiridhisha kuwa miradi yote kumi (10) imetekelezwa kwa kiwango na ubora huku akielekeza kuondolewa kwa changamoto ndogo ndogo zilizobainika katika baadhi ya miradi ambapo amesisitiza kukamilisha kwa wakati miradi ambayo bado inatekelezwa ili iweze kuwanufaisha wananchi.

“ Mbio za Mwenge wa uhuru kwa Mwaka 2023 zimefika katika miradi yetu kwanza kabisa tumepokea taarifa zinazohusiana na miradi baada ya kupokea taarifa tumetembelea tumejionea tumekagua shughuli mbalimbali zinazohusiana na miradi sambamba na kukagua nyaraka mbalimbali zinazohusiana na miradi hiyo”

“Upande wa nyaraka zimepangwa vizuri na tumekagua tumejiridhisha pamoja na ukaguzi ambao tumefanya kwa upande wa miradi viwango vimezingatiwa niseme hongereni sana  kwa kazi nzuri mwenge wa uhuru umeridhi”.amesema Abdalla Kaim

Katika Manispaa ya Shinyanga Mwenge wa uhuru  umekimbizwa umbali wa kilomita 72.5 ambapo umefungua na kuweka mawe ya Msingi  kwenye miradi kumi ya Maendeleo yenye zaidi ya Bilini mbili, ikiwa ni pamoja na kukagua hifadhi ya mazingira,klabu ya wapinga rushwa na klabu  ya lishe katika shule ya sekondari ya Rajani iliyopo katika kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga.

Kauli mbiu ya mbio za mwenge kwa Mwaka huu inasema tunza mazingira, okoa vyanzo vya maji kwa ustawi wa viumbe hai na uchumi wa Taifa.

Mkesha wa Mwenge wa uhuru  utakuwa  katika eneo la uwanja wa saba saba Kambarage mjini Shinyanga,utakaofanyika sanjari na shughuli nyingine ikiwemo upimaji afya kwa hiyari,elimu ya uraia kwa jamii  juu ya masuala mbali mbali pamoja na Burudani.

Awali Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akipokea Mwenge wa uhuru upande wa kulia ni mkuu wa Wilaya ya Kishapu.

Share To:

Misalaba

Post A Comment: