9

Wananchi wa Kijiji Cha Engutoto kata ya Mwandeti katika Halmashauri ya Arusha DC Mkoani Arusha wamemtuhumu Mtendaji wa Kijiji hicho kwa Ubadhirifu wa Fedha zaidi ya Million 18.

Wakizungumza wananchi hao katika Mkutano wa Hadhara Kijijini  wamesema fedha hizo zimetokana na nguvu zao, pamoja michango ya  Wadau wa maendeleo na ukodishaji wa Mashamba waliokubaliana kukusanya kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari Kijijini hapo na hili ni baada ya watoto wao kutembea umbali mrefu kufuata Elimu hususani watoto wakike.

Awali akisoma Mapato na Matumizi Mtendaji wa Kijiji hicho Bwana Mosses Levilal amebainisha mapato na matumizi hayo na kukiri kumiliki millioni 14 huku zaidi ya millioni 4 zikitatanisha zilipo .

Japhet Sioni Ni Mwenyekiti wa kijiji hicho ambapo amekiri kuwepo kwa ubadhirifu wa Fedha hizo huku akijitetea kushirikiana na Mwajiri wa Mtendaji huyo kuhakikisha fedha hizo zinapatikana.

Kwa mujibu wa wananchi wamesema mbali na mtendaji kutuhumiwa kwa ubadhirifu wa Millioni 18 Bado  Mwenyekiti naye habaki salama kutokana na kushindwa kusimamia Rasirimali za Kijiji hicho.



Share To:

Post A Comment: