Na Dotto Kwilasa, Dodoma
Ili kuunga mkono juhudi za Serikali Katika kuwezesha vijana kuwekeza kwenye Kilimo biashara,Kampuni ya Vanilla international Limited imezindua Mradi wa kilimo cha Vanilla Mkoani Dodoma (Vanilla village )katika Kitongoji cha Zamahero Kata ya Mayamaya Wilayani Bahi.
Uzinduzi huo umeambatana na utoaji Elimu kwa wananchi wa eneo hilo kuhusu kilimo cha Vanilla Julai 22,2023 katika shamba la kitalu (green House)kubwa ya kilimo hicho inayotumia njia za kisasa.
Akizungumza na Msumba News leo Julai 28,2023 Dodoma,Mkurugenzi Mtendaji na muasisi wa makampuni ya Vanilla international Limited nchini ,Simon Mkondya amesema shamba kitalu
hilo lipo kilomita 40 kutoka katikati ya Jiji la Dodoma barabara kuu ya kwenda Arusha lenye ukubwa wa hekta 125.
Amesema uwekezaji huo unakwenda kugharimu zaidi ya bilioni 30 za kitanzania .
Mkondya amesema,"Uwekezaji huu ni Kutokana na Serikali kuongeze juhudi kutuwezesha wakulima,haya ni mafanikio makubwa kwetu,tunategemea mafanikio mengi zaidi kupitia kilimo ,mategemeo yangu ni kujipanua zaidi hadi kisiwa cha Zanzibar,"amesema
Post A Comment: