Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza kwenye mkutano Mwaka wa mashirika yasiyo ya kiserikali ambao umefanyika leo Julai 5,2023.
Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme ameyakumbusha mashirika yasiyo ya kiserikali NGO's yaliyopo mkoani hapa kuhakikisha yanaendelea kutekeleza miradi inayolenga kulinda na kuheshimu maadili, mila na desturi za kitanzania kwa ustawi wa Taifa.
Ameyasema hayo leo Jumatano Julai 5,2023 wakati akifungua
mkutano wa Mwaka wa mashirika yasiyo ya kiserikali Mkoani Shinyanga, kwa lengo
la kutambua mchango wa mashirika hayo pamoja na kufanya majadiliano
kuhusu ufuasi mzuri wa sheria, kanuni na taratibu katika utekelezaji wa miradi
mbalimbali.
RC Mndeme amesema serikali haitosita kuchukua hatua zaidi za
kisheria kwa shirika lisilo la kiserikali ambalo litabainika kwa makusudi
kujihusisha na miradi ambayo inakiuka maadili, mila na desturi za Kitanzania.
RC Mndeme ametumia nafasi hiyo kuwaelekeza wataalam wa serikali
wa ngazi ya Mkoa na Halmashauri kuhakikisha wanaimarisha uratibu kwenye
mashirika hayo ili kuepuka mrundikano wa mashirika yanayofanya kazi moja katika
eneo moja.
Aidha, akizungumza katika mkutano huo Mwakilishi wa NGO’s
katika Mkoa wa Shinyanga Bwana Venance Muzuka ameiomba serikali ya Mkoa
kuhakikisha inaendelea kuweka mazingira mazuri na rafiki ya utendaji kazi kwa
mashirika hayo, huku akiahidi kuwa mashirika yasiyo ya kiserikali yataendelea
kufanya kazi kwa kufuata sheria, miongozo na taratibu za nchi.
Katika mkutano huo wa
Mwaka wa mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo yanatekeleza majukumu yake Mkoani
Shinyanga pamoja na mambo mengine wameadhimia mambo mbalimbali ikiwemo serikali
kufanya ufuatilia kwa lengo la kutambua uhai wa mashirika yaliyopo ili yaweze
kutoa mchango wa maendeleo Mkoani Shinyanga.
Wameadhimia pia kuwa na vikao
endelevu vya serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali kwa ajili ya kujadili
masuala mbalimbali ya utekelezaji wa shughuli za NGO’s
Pia wameadhimia kuwa, wasajiri
wa NGO’s katika Halmashauri zote Mkoani Shinyanga kuziunganisha NGO’s kubwa na
mashirika madogo ili kujengeana uwezo katika utekelezaji wa majukumu yao.
Msajili wa mashirika, afisa maendeleo ya jamii Mkoa wa Shinyanga
Bwana Tedson Ngwale akitoa semina kwenye
mkutano wa Mwaka wa mashirika yasiyo ya kiserikali Mkoa wa Shinyanga leo
Jumatano Julai 5,2023.
Msajili huyo wa mashirika Bwana Ngwale ameelezea mambo mbalimbali ikiwemo sera na sheria zinazosimamia uratibu wa mshirika yasiyo ya kiserikali, taratibu za usajiri wa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali pamoja na maudhui ya kanuni ya sheria ya NGO’s.
Mwakilishi wa NGO’s katika Mkoa wa Shinyanga Bwana Venance Muzuka akizungumza kwenye mkutano wa Mwaka wa mashirika yasiyo ya kiserikali Mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Julai 5,2023.
Afisa elimu na mawasiliano kwa mlipakodi kutoka TRA Mkoa wa Shinyanga Bi. Semeni Mbeshi akielezea mambo mbalimbali ikiwemo namna ya mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali kulipa kodi ambapo amesema mashirika yanawajibu wa kufuata sheria zote za mlipa kodi.
Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga Bwana Donasian Kessy akizungumza kwenye mkutano huo wa Mwaka wa mashirika yasiyo ya kiserikali Mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Julai 5,2023.
Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kamishna wa Polisi Janeth Magomi akiyaomba mashirika kuendelea kushirikiana katika utekelezaji wa majukumu yao ili kuimarisha usalama.\
Mwenyekiti wa kamati ya amani na maridhiano Mkoa wa shinyanga Shekh Balilusa Khamis akiwasihi kuzingatia maadili na kushirikiana pamoja katika kutokomeza vitendo vya ukatili.
Mkutano wa Mwaka wa mashirika yasiyo ya kiserikali Mkoa wa Shinyanga ukiendelea leo Jumatano Julai 5,2023 katika ukumbi wa mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Mkutano wa Mwaka wa mashirika yasiyo ya kiserikali Mkoa wa Shinyanga ukiendelea leo Jumatano Julai 5,2023 katika ukumbi wa mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Mkutano wa Mwaka wa mashirika yasiyo ya kiserikali Mkoa wa Shinyanga ukiendelea leo Jumatano Julai 5,2023 katika ukumbi wa mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Mkurugenzi wa Shirika la Youth Adivisory Development Council
(YADS) akitoa maoni kwenye mkutano wa Mwaka wa mashirika yasiyo ya kiserikali ya
Mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Julai
5,2023.
Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la ICS Mkoa wa Shinyanga Bwana Kudely Sokoine Joram akitoa maoni kwenye mkutano wa Mwaka wa mashirika yasiyo ya kiserikali ya Mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Julai 5,2023.
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Agape Mkoa wa
Shinyanga Bwana John Myola akitoa maoni kwenye mkutano wa Mwaka wa mashirika yasiyo ya
kiserikali ya Mkoa wa Shinyanga leo
Jumatano Julai 5,2023.
Meneja wa shirika la Chidep Mkoa wa Shinyanga Bwana
Nashon Peter akitoa
maoni kwenye mkutano wa Mwaka wa mashirika yasiyo ya kiserikali ya Mkoa wa Shinyanga
leo Jumatano Julai 5,2023.
Mwenyekiti wa Asasi ya Wanawake Laki
Moja Anascholastica Ndagiwe akitoa maoni kwenye mkutano wa Mwaka wa mashirika yasiyo ya
kiserikali ya Mkoa wa Shinyanga leo
Jumatano Julai 5,2023.
Mwenyekiti wa taasisi ya msaada wa kisheria Mkoa wa Shinyanga Bwana John Shija akitoa maoni kwenye mkutano wa Mwaka wa mashirika yasiyo ya kiserikali ya Mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Julai 5,2023.
Mkurugenzi wa Shirika la Fikra Mpya Leah Josiah akitoa maoni kwenye mkutano wa Mwaka wa mashirika yasiyo ya kiserikali ya Mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Julai 5,2023.
Post A Comment: