Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mwalimu Alexius Kagunze amesema miradi kumi ya maendeleo itazinduliwa, kufunguliwa na kuwekwa mawe ya msingi na Mwenge wa uhuru Julai 28, 2023 Mwaka huu.

Amesema maandalizi yamekamilika kwa asilimia mia moja huku akitaja miradi itakayotembelewa  na Mwenge wa uhuru ikiwa ni pamoja na kupanda miti, kukagua clabu ya Rushwa na clabu ya lishe katika shule ya sekondari Rajani kata ya Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga.

Amesema mwenge wa uhuru utafungua ujenzi wa madarasa sita (6) na ofisi mbili (2) za walimu katika shule ya msingi Bugweto na kwamba mradi huo unathamani ya Shilingi Milioni 40.

Mwalimu Kagunze amesema Mwenge wa uhuru utakagua mradi wa asilimia 10 wa magari mawili ya vijana ya abiria ambapo pia utafanyika ukaguzi wa shughuli za vijana za usafi na utunzaji wa mazingira, kushiriki usafi pamoja na kutoa cheti cha pongezi huku akitaja mradi huo kugharibu zaidi ya Miliani mia moja kwa vijana wa mtaa wa Kalogo kata ya mjini Manispaa ya Shinyanga.

Mkurugenzi huyo amesema pia utazindua chuo cha serikali za mitaa kampasi ya Shinyanga kilichopo jingo la SHIRECU ambapo mradi huo unagharimu  zaidi ya Miliani mia moja.

Mradi mwingine utakaowekewa jiwe la msingi ni ujenzi wa madaraja mawili kata ya Kitangili nao unagharibu zaidi ya shilingi Milioni mia moja pamoja na kuzindua mradi wa maji Bugayambelele kata ya Kizumbi wenye unaogharimu zaidi ya Milioni mia mbili.

Mwenge huo pia utaweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa soko la Ibinzamata, kukagua hifadhi ya mazingira NAFRAC Bushushu kata ya Lubaga, kuzindua mradi wa kiwanda cha maziwa Mwalugoye kata ya Chibe.

Pia Mwenge wa uhuru utafungua OPD, wodi ya wazazi, jingo la mionzi na njia za watembea kwa miguu pamoja na kugawa neti, kukagua upimaji wa malaria na dawa za kulevye katika kituo cha Afya Kambarage mjini Shinyanga.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mwalimu Alexius Kagunze amewaomba wakazi wa Manispaa ya Shinyanga kujitokeza kwa wingi  ambapo amesema mkesha wa Mwenge wa uhuru  utafanyika uwanja wa saba saba Kambarage mjini Shinyanga.

Share To:

Misalaba

Post A Comment: