Mbunge wa viti maalum mkoa wa Lindi kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Tecla Mohamed Ugele akiongea na wananchi wa wilaya ya Nachingwea katika mkutano ulioitishwa na mbunge wa Jimbo la Nachingwea Dr Amandus Chinguile
Na Fredy Mgunda, Nachingwea.
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Lindi kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Tecla Mohamed Ugele amewaomba wananchi wote mkoa wa Lindi kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Samia suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuleta maendeleo Kwa watanzania.
Ugele aliyasema hao wakati wa mkutano wa hadhara uliokuwa umeandaliwa na mbunge wa Jimbo la Nachingwea Dr Amandus Chinguile katika kata ya Nachingwea.
Alisema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Samia suluhu Hassan amefanya kazi ambayo inaonekana kwa kila mtanzania na ambaye sio mtanzania kwa kufungua fursa mbalimbali kwa watanzania.
Mbunge Ugele aliwataka wananchi kuwapuuza wanasiasa,wanasheria na wanaharakati wanaopiga uwekezaji katika bandari ya Dar es salaam kuwa uwekezaji hauna tija hivyo amesema kuwa uwekezaji unatija kubwa kwa watanzania katika kukuza uchumi na maendeleo ya Tanzania.
Alisema kuwa Nachingwea ya leo imebadirika sana kimaendeleo tofauti na Nachingwea ya miaka miwili iliyopita hivyo alimpogeza mbunge wa Jimbo hilo Dr Amandus Chinguile pamoja Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Samia suluhu Hassan kwa kupeleka maendeleo Kwa watanzania wanaoishi na kupita Jimbo la Nachingwea.
Alisema kuwa katika wilaya ya Nachingwea Rais Dr Samia suluhu Hassan amepeleka fedha nyingi katika sekta ya barabara,afya, elimu,miundombinu na kilimo jambo ambao kila mwananchi wa Nachingwea anaona mabadiliko hayo hivyo ni vizuri watanzania wakaendelea kumuunga mkono Rais kwa ambazo anazifanya za kimaendeleo.
Post A Comment: