Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde ameahidi kujenga jengo la darasa moja na kukarabati viwanja vya michezo vya Shule ya Msingi Iyumbu,Jijini Dodoma.
Mbunge Mavunde ameyasema hayo jana wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza Timu ya Garden FC ya Iyumbu ambayo iliyotangazwa kuwa bingwa wa FANUEL CUP 2022/23
“Ninawapongeza sana Vijana wote wa Iyumbu kwa kushiriki katika michezo kwa lengo ya kuendeleza vipaji vyenu na kutumia michezo hii kama fursa ya Ajira.
Nimesikia risala yenu juu ya ombi la ukarabati wa uwanja huu mnaouchezea,nitaka kuwahakikishia kwamba nitaufanyia matengenezo uwanja huu mapema kabisa ili uweze kuchezeka kiurahisi.
Nilikuja hapa miaka kadhaa na nilianzisha msingi na kuchangia ujenzi wa madaraa matatu ambayo naona yanaendelea vizuri.Pamoja na hayo nitawatafutia fedha za ujenzi wa darasa moja jipya ili kuongeza idadi ya vyumba vya madarasa”Alisema Mavunde
Naye Diwani wa kata ya Iyumbu Elias Sutuchi amemshukuru Mbunge Mavunde kwa ushirikiano mkubwa katika kuwaletea maendeleo wananchi wa kata ya Iyumbu ikiwa na pamoja kuwa chachu ya kuhamasisha michezo katika kata hiyo.
Post A Comment: