NA DENIS CHAMBI, TANGA.
JESHI
la Polisi mkoa wa Tanga limefanikiwa kuwakamata watu kumi na moja
wakiwemo wanawake wawili na wanaume tisa wakazi wa Dar es salaam
waliokuwa wakijihusisha na wizi wa fedha kwa njia ya simu ambapo
wamekuwa wakituma ujumbe kwa watu mbalimbali wakiwataka wawatumie
fedha bila ridhaa yao.
Akitoa
taarifa hiyo kwa vyombo vya habari kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa
Tanga Henry Mwaibambe amesema kuwa watuhumiwa wote walikuwa wakiishi
katika nyumba moja waliyokuwa wamepanga maeneo ya Donge Kata ya
Mnyanjani jijini hapa ambapo wote wamefikishwa mahakamani kujibu tuhuma
zinazowakabili.
Kamanda
Mwaibambe aliongeza kuwa watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa na vitu
mbalimbali ikiwemo laini za simu 42 vocha mbili zenye thamani ya
shilingi 2,000 karatasi 43 zilizoandikwa namba za simu na namba za
mawakala wa mitandao ya fedha, kadi tano za benki mbalimbali,
vitambulisho 14, na betri za simu ndogo 7.
Aliwataja
watuhumiwa hao kuwa ni Hadija Nyange (34) mkazi wa Muheza, Zaina
Athuman (25) mkazi wa Mwazange, Innocent Omeme (35),Abdulazizi Nzori
(31),Said Hassan (24), Rashid Habibu (23), Said Juma (30), Idd Kaniki
(35), David Rupiana (22), Salum Salum (24) wote wa kutoka Dar es salaam
pamoja na Omary Mohammed (27) mkazi wa Mkanyageni Tanga ambapo wote
wamefikishwa mahakamani.
"Jeshi
la Polisi mkoa wa Tanga limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 11 ambao
wanajihusisha na uhalifu kwa njia ya mtandao ambao hutuma ujumbe mfupi
wa maneno kwa watu mbalimbali wakiwataka watume pesa, baada ya kukamatwa
walikutwa na fedha tathlimu milion mbili na elfu themanini na tani
(2,085,000), pesa ya Congo elfu arobaini na tano na mia moja (450,100) ,
simu kubwa 11, simu ndogo 13 kadi 5 za benki mbalimbali, " alisema
"Aidha
katika ufwatiliaji jumla ya laini za simu 441 walizokuwa nazo
watuhumiwa kwa lengo la kuwatapeli watu mbalimbali kwa kuziorodhesha
namba za simu na majina ya watumiaji, laini 399 za simu baada ya kufanya
utapeli walizichoma moto na kati ya laini hizo 183 zilitumiwa ujumbe
mfupi wa maneno na kumtaka mwananchi atume pesa , laini 42 za simu
zilikuwa katika mchakato wa kuwatapeli watu mbalimbali watuhumiwa hao
wamefikishwa mahakamani kujibu mastaka yanayowakabili" alisema Kamanda
Mwaibambe.
Hata hivyo
Kamanda Mwaibambe amewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa
jeshi la Polisi ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu
pale wanapowaona katika maeneo yao ili kuendelea kudumisha amani na
usalama nyakati zote.
"Hawa
watu ni watu hatari sana tusiposhirikiana na jeshi la Polisi hatuwezi
kuwafunga wakitoka hapa wanaweza kwenda kutapeli na kwingineko, tunaomba
sana mtoe ushirikiano katika kukomesha vitendo hivi" aliongeza.
Katika
hatua nyingine kwenye barabara ya Same maeneo ya Chekelei mkoani Tanga
jeshi hilo limefanikiwa kukamata watu watatu wakiwa na gari waliokuwa
wamebeba bunda 313 za madawa ya kulevya aina ya Milungi zenye uzito wa
kilo 112.05.
"Jeshi la
Polisi mkoa wa Tanga tunaendelea na juhudi za kupambana na madawa ya
kulevya , tumefanikiwa ndani ya mwezi huu wa 7 barabara ya Tanga
kwenda Same maeneo ya Chekelei tuliweza kukamata watuhumiwa watatu
wakiwa kwenye gari zenye usajili namba T 417 CJS walikutwa wakiwa ndani
na madawa ya kulevya aina ya Milungi bunda 313 zenye uzito wa kilo
112.05 tayari taratibu za kisheria zishafanyika kielelezo tumepeleka
kwa mkemia mkuu wa serikali amethibitisha kuwa ni madawa ya kulevya aina
ya Milungi" alisema Kamanda
Post A Comment: