Julieth Ngarabal. Pwani
Malipo kwa njia ya Dirishani (keshi) kwa Wanufaika wa mradi wa kuondoa umasikini TASAF ni njia halali na kwamba Wananchi wote waliopo kwenye mpango huo ni ruksa kutumia kama ilivyo kwa njia zingine za ki benki kwa wenye akaunti na njia ya mtando kwa wenye simu.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete amesema njia tatu zote hizo ni halali kwa malipo na ndio zilzokubalika katika utaratibu wa TASAF na kueleleza ziendelee kutumika kulipa wanufaika kama ambayo imeelekezwa
Ridhiwani ametoa maelekeza hayo wakati akizungumza na Watendaji na Wanufaika wa Mradi wa kuondoa Umasikini TASAF huko Mtaa wa Miwaleni mjini Kibaha Mkoani Pwani
"Msije mkaleta maneno au janja janja hapa matokeo yake siku tukaingia kwenye shida ya kuwatia dhiki Wananchi wetu,na kama upo utaratibu wowote ambao unakwama ndugu Wananchi Serikali yenu sikivu ya Dk. Samia Suluhu Hassan inasema leteni malalamiko sisi tupo tuyafanyie kazi"amesema Ridhiwani.
Pia amewataka watedaji Kibaha wasiwasubiri Wanufaika wa mradi huo wao ndio waende kwenye Ofisi za kata huku wanajulikana , na wasitafute kisingizio cha kutowasaidia wa Tanzania maana Rais Dk. Samia alishatoa maelekezo wanufaika watambuliwe.
Naibu Waziri huyo amewahakikishia utayari wa Serikali kuendelea kupambana kuhakikisha inamfikia kila mtanzania mwenye hali ya Umaskini na kuwa itahakikisha inabadili maisha yao
Mapema kabla ya kuwatembelea wanufaika wa TASAF, Ridhiwani alianza kuzungumza na watumishi wa Serikali ngazi ya Mkoa na wa Halmashauri ya Mji Kibaha ambapo amewaasa kuacha tabia ya kusemana ovyo ,kuwekeana fitna ,na kufanyiana vituko kwani kwa kufanya hivyo ni kuzorotesha utendaji kazi kwenye maeneo yao.
Pia Ridhiwani amewataka kila mtumishi kutimiza wajibu wake na wawe wabunifu kwenye utendaji kazi sambamba na maofisa Utumishi wafanye kazi kwa uadilifu ili kupunguza malalamiko yasiyo ya lazima kwa watumishi.
"Hili ni eneo muhimu ,shughulikieni matatizo ya watumishi,ondoeni malalamiko ya Utumishi na kuwashauri kama kuna sintofahamu ili kushirikiana na kuweza kufanya mambo yaende vizuri"
Awali Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge ameongeza watumishi Mkoani humo wana wajibu wa kutekeleza mipango ya maendeleo na kuondoa kero za wananchi ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya chama cha Mapinduzi (CCM)
Baadhi ya kero kutoka kwa watumishi ni pamoja na kupandiishwa madaraja, , asilimia 33 ya mafao iondolewe na badala yake mtumishi akistaafu apewe fedha zake zote,
Post A Comment: