Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya imekutana kwa lengo la kujadiliana mambo mbalimbali ikiwemo ujenzi wa ofisi mpya ya Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Chunya.
Katika kikao hicho Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi kwa kushirikiana na Mbunge wa Lupa Mheshimiwa Masache Kasaka wameahidi kuchangia shilingi milioni ishirini na tano kila mmoja na Madiwani kila Kata kuchangia shilingi milioni mbili ili kukamilisha ujenzi wa ofisi mpya ya Chama itakayokuwa na ukumbi wa mikutano sambamba na ofisi za jumuia zote za Chama.
Kikao hicho kiliongozwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Chunya Noel Chiwanga pia kuhudhuriwa na Kamisaa wa Wilaya ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya Mayeka Simon Mayeka.
Post A Comment: