NA DENIS CHAMBI, TANGA.

NANI atakwenda kunyakua taji la ligi ya mpira wa kikapu mkoa wa Tanga msimu huu?  Pengine hili ni swali ambalo wanafamilia wa mchezo huo wanajiuliza ambapo utepe wa michauano hiyo utakwenda kukatwa July 29 huku viwanja vya Korogwe na Mkwakwani Tanga vikitumika kwa michauano hiyo.

Michauano  hiyo  ambayo mwaka huu itajulikana kwa jina  'TRBA'  Mkonge City Basket ball ligi  itahusisha timu 6 za wanaume zitakazoingia katika kinyang'anyiro  hicho ambazo ni Tanga United, Deep sea ( Harbours  Club),
Ng'e, Korogwe Heat, Bandari Tanga pamoja na  Ngamiani  Kings.

Akizungumza katibu wa chama cha mpira wa Basketball mkoa wa Tanga Riziki Mgude amesema kuwa maamuzi waliyofanya kucheza ligi hiyo katika viwanja viwili vya wilaya tofauti ni mpango wao wa kuzidi kuongeza  hamasa na wigo mpana wa mchezo huo katika wilaya zote zilizopo sambamba na kuipa Korogwe Heats thamani kuipunguzia safari za kwenda na kurudi kwaajili ya kuweza kushiriki.

"Ligi ya mpira wa Kikapu mwaka huu itajulikana kama TRBA Mkonge City Basketball ligi  inatarajiwa kuanza July 29 ambapo wikiendi hii ya tarehe 23 tutakutana kwaajili ya mechi ya ufunguzi na mwaka huu tuna timu 6 mwaka jana tulikuwa na timu 4 na viwanja vitakavyoyumika vitakuwa ni viwili vya Mkwakwani na Korogwe , tutacheza mizunguzo miwili halafu wale wawili wa juu watakwenda kucheza fainali" alisema Mgude.

Katibu huyo amesema kuwa kuna maboresho makubwa wameyafanya katika upande wa zawadi kwa washindi wa michauano hiyo msimu huu ukitofautisha na ule wa mwaka 2022 hii ikilenga hasa kuongeza chachu ya ushindani kwa timu zote zitakazochuana kumtafuta bingwa wa 2023.

" Ni matumaini yetu kwamba zawadi zitakuwa lukuki mwaka jana tulitoa vikombe viwili kwa kila mshindi na medal kwa mshindi wa kwanza na wa pili mwaka huu tunataka tuongeze zawadi nyingine ili ligi ipate thamani na kila timu itayoa kiingilio cha shilingi laki mbili  na bado tupo kwenye mchakato wa kutafuta wadhamini ili kutuongezea thamani ligi yetu" aliongeza Mgude.
 

Mabingwa watetezi wa kombe la ligi ya Mpira wa kikapu mkoa wa Tanga Bandari Tanga  kwa mwaka 2022
Kikosi cha timu ya Korogwe heats  kitakachoshiriki 'TRBA'  Mkonge City Basket ball ligi mwaka huu 2023.
Kikosi cha timu ya Habours Club(Deep see) kitakachoshiriki 'TRBA'  Mkonge City Basket ball ligi mwaka huu 2023.



Share To:

Post A Comment: