Ni katika ziara ya Mwenyekiti wa jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Monduli katika kata ya Lashaine.

Hii inakuja baada ya uchaguzi wa Mwaka Jana wa Chama na Jumuiya zake Wilayani Monduli ambapo Mwenyekiti huyo aliahidi kufanya ziara Kila kata  ,ambapo alianza rasmi February mwaka huu katika kata ya Lemooti , na hii Leo amemaliza ziara yake kata ya Lashaine baaada ya sababu zilizopo nje ya uwezo kuhairishwa kwa ziara hiyo.

Ndugu kisioki Moitiko amesema Nia yake na Matumaini yake katika jumuiya ni kupata wanachama wengi lakini pia Jumuiya hiyo kujitegemea kiuchumi hasa kupitia miradi mbalimbali ikiwemo vikundi vya kina mama.


" Nilitamani sana hii ziara katika kata hii niseme TU kuwa Leo nimekuja kutimiza Ahadi yangu niliyoitoa wakati naomba kura kwamba lazima nifike kufanya ziara Kila kata , nawashukuru sana mama zangu kwa mapokezi yenu,  baba zangu , kaka zangu na wananchi wa Lashaine Kwa ujumla na vikundi vya kina mama , itoshe kusema jumuiys hii ni uhai na wingi wa wanachama lakini pia Nia yangu na kiu yangu ni Jumuiya hii kujitegemea kiuchumi kupitia miradi mbalimbali hasa vikundi vya kinana , hapa kuna vikundi zaidi ya nane , mwenyekiti wa chama na jumuiya hii ya wazazi jumatatu njoo ofsini kwangu chukueni millinioni 4 kwa ajili ya kuwasapoti kina mama Hawa na niahidi tu kwa kikundi kitakachofanya vizuri katika uwekezaji tutawasapoti kwa njia yeyote Ile " Kisioki moitiko


Aidha kwa upande wake Katibu wa jumuiya hiyo Bi Bitrice Mandia amewasisitizia viongozi wa jumuiya hiyo kuanzia matawi kufanya vikao kwani uhai wa jumuiya ni vikao, huku Katibu wa malezi na mazingira Wilayani humo mh Thomas Meiyan , amesema Jumuiya hiyo inasimamia mambo Matano ikiwemo Elimu, Mazingira, Malezi, Afya na Uchumi, na kuwasisitiza wazazi kuwapeleka watoto shule pamoja na kina mama kuhudhuria kliniki Kwa wakati.


Katika ziara hiyo ya Jumuiya ya Wazazi  Mwenyekiti huyo aliongozana na Katibu wa CCM Monduli Bi Rukia Mbasha Ambapo , Amewasihi vijana kuacha kutumika na wanasiasa  kwani wanaharibu Taswira ya Chama , na kusema kipindi Cha Uchaguzi Bado waache viongozi walipo madarakani kufanya kazi zao.


" Vijana mnatumika sana Acheni hizo mnaharibu hadi tamaduni zenu kwa kuwatukana wakubwa wenu kisa siasa na kutumika vibaya, hii nchi ina Raisi mmoja TU Mama Samia Suluhu Hassan, Hili Jimbo Lina Mbunge mmoja TU Fredrick Lowassa, hii kata Ina Diwani mmoja TU Mh Grosper Mollel, Hii Kijiji Ina mwenyekiti mmoja tu huyu tunayemuona hapa , tuacheni siasa tufanye kazi  wewe unayetaka nafasi subiri kipindi cha uchaguzi ufike na wewe ukagombeee, Mwisho Diwani ameeleza miradi ya Maendeleo hapa Ikiwemo maji, umeme, Zahanati nk hizi zote zimetekelezwa na chama cha CCM tuendelee kuwaamini viongozi wetu , tuwape nafasi wafanye kazi siasa ni baadaye" Rukia Mbasha

Share To:

Post A Comment: