Wakazi wa kata za Mpepo, Mipotopoto, Lumeme na Uhuru zilizopo Wilayani Nyasa Mkoani Ruvuma wamepewa uhakika wa kupata huduma ya majisafi, salama kupitia miradi ya maji itakayotekelezwa maeneo hayo.
Naibu Waziri wa Maji Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) amesema Serikali itatekeleza miradi ya maji kwenye kata hizo ambapo kata ya Lumeme (kijiji cha Mbanga) kwa mwaka wa fedha 2023/24 jumla ya shilingi milioni 224 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa maji kijijini hapo.
Amesema Serikali inaendelea kutafuta vyanzo vya maji vya uhakika ambavyo vitatumika wakati wa utekelezaji wa miradi hiyo.
Mhe. Mahundi ametoa ufafanuzi huo wakati wa ziara ya kikazi inayoendelea Mkoani Ruvuma ya Mwenyekiti wa Umoja Wanawake Tanzania (UWT) Taifa.
Audha, Mhe. Mahundi ameeleza kuwa kwenye Wilaya ya Nyasa Serikali inaendelea na utekelezaji wa miradi mitano yenye thamani ya shilingi Bilioni 16.9 ambapo utekelezaji wa miradi hiyo ipo katika hatua mbalimbali
Kwa upande wake Mheshimiwa Mhandisi Stella Manyanya Mbunge wa Jimbo la Nyasa ameishukru Wizara ya maji kwa kuendelea kutekeleza miradi ya maji mbalimbali kwenye Jimbo la Nyasa.
Post A Comment: