Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Kamati ya fedha na utawala kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mwalimu Alexius Kagunze leo Jumamosi Julai 22,2023 wamefanya ziara kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika Manispaa ya Shinyanga.

Miradi iliyotembelewa ni ujenzi katika shule ya sekondari Old Shinyanga, ujenzi wa shule ya wasichana Butengwa kata ya Ndembezi, ujenzi wa madarasa shule ya msingi mpya Ibadakuli, ujenzi wa jengo la wagonjwa wa dharura (EMD) Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga pamoja na ujenzi wa jengo la utawala Manispaa ya Shinyanga.

Akizungumza baada ya ziara hiyo Mwenyekiti wa kamati ya fedha na utawala ambaye pia ni Mstahiki meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko amepongeza kwa hatua nzuri iliyofikiwa katika utekelezaji wa miradi hiyo.

Mwenyekiti huyo amesema kamati imefurahishwa na hatua iliyifikiwa katika miradi hiyo ambapo ameahidi kuendelea kusimamia mipango iliyokusudiwa na serikali kupitia ilani ya chama cha mapinduzi CCM.

Mhe. Masumbuko ametumia nafasi hiyo kumpongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo Manispaa ya Shinyanga kupitia sekta mbalimbali ikiwemo Afya, Elimu pamoja na sekta ya Maji.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mwalimu Alexius Kagunze serikali itaendelea kuweka msukumo katika miradi inayoendelea ili iweze kukamilika kwa wakati.

Mkurugenzi Mwalimu Kagunze amesema miradi yote inayotekelezwa katika Manispaa ya Shinyanga imelenga kutatua changamoto zilizopo pamoja na kuchochea uchumi kwa wananchi, Halmashauri na Taifa kwa ujumla.

Mwalimu Kagunze naye amempongeza na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassani kwa kuendelea kutoa fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Manispaa ya Shinyanga huku akiahidi kusimamia vyema miradi yote ya maendeleo.

Amewata mafundi kuongeza kasi kwenye ujenzi ili miradi hiyo iweze kukamilika kwa wakati ambapo amesema ataendelea kutoa ushirikiano katika utatuzi wa changamoto zilizopo.

Kaimu wa Division ya miundombinu na maendeleo ya miji na vijiji Manispaa ya Shinyanga Mhandisi Kassim Thadeo  ameahidi kutekeleza maelekezo yaliyotolewa na kamati ya fedha na utawala kwenye miradi ya maendeleo kutekelezwa.

Kamati ya fedha na utawala kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mwalimu Alexius Kagunze leo wamefanya ziara kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo wakiambatana na wataalam mbalimbali wa  Manispaa ya Shinyanga.

Muonekano wa hatua zilizofikiwa za ujenzi katika shule ya sekondari Old Shinyanga.

Kamati ya fedha na utawala kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mwalimu Alexius Kagunze wakiwa katika zoezi la kukagua ujenzi katika shule ya sekondari Old Shinyanga leo Jumamosi Julai 22,2023

Kamati ya fedha na utawala kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mwalimu Alexius Kagunze wakiwa katika zoezi la kukagua ujenzi kwenye shule ya sekondari Old Shinyanga leo Jumamosi Julai 22,2023

Kamati ya fedha na utawala kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mwalimu Alexius Kagunze wakiwa katika zoezi la kukagua ujenzi kwenye shule ya wasichana Butengwa kata ya Ndembezi  leo Jumamosi Julai 22,2023

Kamati ya fedha na utawala kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mwalimu Alexius Kagunze wakiwa katika zoezi la kukagua ujenzi wa jengo la wagonjwa wa dharura (EMD) Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga  leo Jumamosi Julai 22,2023

Kamati ya fedha na utawala kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mwalimu Alexius Kagunze wakiwa katika zoezi la kukagua ujenzi wa shule ya msingi mpya Ibadakuli leo Jumamosi Julai 22,2023

Viongozi wakipokea taarifa.

Muonekano madarasa katika shule ya msingi Ibadakuli.

Kamati ya fedha na utawala kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mwalimu Alexius Kagunze wakiwa katika zoezi la kukagua ujenzi wa jengo la utawala Manispaa ya Shinyanga leo Jumamosi Julai 22,2023

Share To:

Misalaba

Post A Comment: