KAIMU Katibu Tawala Mkoa wa Pwani (RAS), Bi. Salvera Salvatory ameishauri Bohari ya Dawa (MSD) kuwa na mikakati endelevu ya kuboresha upatikanaji wa bidhaa za afya ili kuondoa malalamiko kwa wananchi ambayo kwa kiasi kikubwa yameanza kupungua. Bi Salvatory ameyasema hayo wakati akifungua mkutano wa MSD Kanda ya Dar es
Salaam na wadau wake wa Mkoa wa Pwani uliofanyika Kibaha Julai 6, 2023. “Wananchi wanafarijika sana wanapofika kwenye vituo vya kutolea huduma za
afya wakapatiwa Dawa zote walizoandikiwa” Kiongozi huyo amekiri kuvutiwa na MSD kuwa na kitengo cha Huduma kwa
Wateja, ambao ndio hufanya mawasiliano kwa karibu na wadau na wateja, ambapo
amewashauri kuhakikisha wanafuatilia malalamiko ya wateja na namna
yanavyoshughulikiwa. Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji na Miradi wa MSD Victor Sungusia
ameeleza kuwa usambazaji wa bidhaa za afya mara sita kwa mwaka umesaidia
kuongeza hali ya upatikanaji wa bidhaa hizo kwenye vituo vya kutolea huduma za
afya nchini. Kwa upande wake Meneja wa Kanda ya MSD Betia Kaema ameahidi kufanyia kazi
maazimio yote yaliyoazimiwa kwenye kikao hicho huku akisisitiza ushirikiano na
mawasiliano ya mara kwa mara na wadau hao. |
Wadau wa MSD wakiwa kwenye mkutano huo
Mkutano ukiendelea |
Post A Comment: