Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga linawashikilia watuhumiwa wanne ambao wanaosadikiwa kuhusika na mtandao wa wakata mapanga katika maeneo mbalimbali.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga, kamishina msaidizi wa Polisi Leonard Nyandahu amesema watuhumiwa hao wamekamatwa kati ya Juni 22 hadi Julai 25 mwaka huu kupitia misako na oparesheni mbalimbali kwa lengo la kuzuia uhalifu na kuuweka Mkoa katika hali ya utulivu.

Amesema watuhumiwa hao wamekiri kufanya matukio ya kukata watu mapanga katika maeneo mbalimbali na kwamba mmoja kati yao amekuwa akiwadhamini wenzake kwenda kutekeleza uhalifu huo.

Aidha, Kaimu Kamanda Nyandahu amesema katika kipindi hicho jeshi hilo limefanikiwa kukamata vitu na vielelezo mbalimbali ikiwemo bunduki tano ambazo zilikuwa zinakodishwa kwa watu wengine na makampuni ya ulinzi jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

“Tumekamata bunduki nne aina ya rifle ambazo zilikuwa zikitumika katika makampuni ya ulinzi na kuazimana kinyume na sheria, tumekamata risasi 73 za shotgun, maganda 13 ya risasi za shotgun, risasi za pisto 239, pikipiki mbili, Bangi kilo mbili na kete mbili, cappet vipande 2, waya wa fensi mita 12, mali idhaniwayo kuwa ni mali ya mgodi wa Buzwagi, mafuta ya diseal lita 310, matairi 5 ya roli yaliyoibiwa katika mradi wa reli SGR na vifaa vya kupigia ramli chonganishi”.amesema Nyandahu

“Kesi 33 za makossa ya jinai zikiwa na jumla ya washitakiwa 41 ziliweza kupata mafanikio mbalimbali mahakamani ambapo kesi moja kati ya hizo niya kujeruhi mtuhumiwa mmoja mwenye miaka 27 mkazi wa Shuni Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga alihukumiwa Miaka kumi jela na akitoka alipe pesa shilingi laki moja”.amesema Nyandahu

Jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga linaendelea kutoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana katika kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu pia kufuata sheria za Nchi kwa kutojihusishana na vitendo hivyo.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga, kamishina msaidizi wa Polisi Leonard Nyandahu akitoa taarifa yake kwa waandishi wa habari, leo Jumatano Julai 26,2023.


Share To:

Misalaba

Post A Comment: