Ushauri huo wa kuhimiza ushirikiano katika mapambano ya kuondoa Umaskini umetolewa na Naibu Waziri wa Utumishi na Utawala Bora Ndg. Ridhiwani Kikwete alipokuwa anaongea na wanufaika wa mradi huo katika kijiji cha Kisanga, Kata ya Masaki Wilayani Kisarawe.
Akiongea katika mkutano huo Ndg. Kikwete amewaasa watendaji kusimamia na kuzingatia vigezo wakati ili kuwatambua wanufaika wa mradi na kuhakikisha haki inatendeka wakati wa zoezi la utambuzi ili nia ya serikali kuwatoa wananchi katika hali ya umaskini inafanikiwa.
Pamoja na hatua hizo , Mh. Naibu Waziri alionyesha umuhimu wa wadau wote ikiwemo Halmashauri kushirikiana na mradi huu wa TASAF ili kufanikisha nia hii ya serikali haswa baada ya TASAF kuwatoa katika hatua ya Mwanzo. Hii inatokana na ukweli kuwa mfumo huu wa TASAF umeonyesha mafanikio makubwa sana.
Post A Comment: