Naibu Katibu Mkuu Ofisi  ya Rais  Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI (ELIMU) Dk. Charles Msonde (katikati), akizungumza na Wanafunzi wa Sekondari ya Mwanzi iliyopo Manyoni mkoani hapa wakati wa siku ya kwanza ya ziara yake ya kikazi ya kutembelea na kukagua ujenzi wa shule kupitia mradi wa BOOST aliyoianza jana Julai 9, 2023.

......................................................

Na Dotto Mwaibale, Singida

NAIBU Katibu Mkuu Ofisi  ya Rais  Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI (ELIMU) Dk. Charles Msonde amezihimiza Halmashauri za Wilaya kote nchini kukamilisha miradi ya ujenzi wa shule zinazojengwa kwa fedha za BOOST ili Tanzania iwe nchi ya mfano kwa mataifa mengine kuja kujifunza mafanikio ya sekta ya elimu kutokana na kukamilika kwa miradi hiyo kwa kiwango cha juu.

Dk. Msonde ameyasema hayo leo Julai 9, 2023 wakati alipotembelea miradi ya ujenzi wa shule za msingi na sekondari za Halmashauri za wilaya za Manyoni, Itigi, Ikungi na Singida.

Msonde alisema Halmashauri zihakikishe zinakamilisha miradi ya BOOST ifikapo Julai 30, 2023 ili wanafunzi wajiunge katika shule na kuanza kutumia majengo hayo.

'Tanzania itakuwa nchi ya mfano katika uboreshaji wa miundombinu ya shule na nina amini kwa nchi nyingine za Afrika na mataifa mengine yatakuja kujifunza kuona jinsi tulivyofanikiwa kutokana na kazi kubwa na nzuri aliyoifanya Rais wetu Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi kwenye sekta ya elimu," alisema Dk.Msonde.

Alisema fedha zilizopokelewa kwa awamu ya kwanza  ambazo zimetolewa kama mkopo na Benki ya Dunia (WB) kwa ajili ya kutekeleza mradi huo  wa BOOST kwa miaka mitano ni  Sh. Trilioni 1.15 na umelenga kuimarisha ujifunzaji katika elimu ya awali na msingi.

Dk.Msonde alisema kumekuwa na ongezeko kubwa la wanafunzi wanao maliza kidato cha nne kwenda cha tano na sita hivyo kwa kuwa Serikali ni sikivu ikaona ni vema kujenga shule hizo kwa ajili ya wanafunzi hao.

Katika ziara hiyo Dk.Msonde alizipongeza halmashauri za Manyoni, Ikungi na Singida kwa kuzisimamia vizuri fedha hizo na kutekeleza miradi hiyo kwa viwango na kwa wakati na akahimiza kuongeza kasi zaidi iliikamilike ndani ya muda uliopangwa.

"Nawaombeni ongezeni kasi ya kukamilisha mradi huu kwa kuweka mafundi wengi ambao watakuwa wakishambulia kila kona badala ya kusubiri mafundi waliopo kufanya kazi hiyo peke yao huku kasi yao ikiwa ndogo," aliongeza Msonde.

Baadhi ya shule alizotembelea na kukagua ujenzi huo ni Shule ya Sekondari ya Mwanzi iliyopo Manyoni, Shule mpya ya Msingi ya Igonoa iliyopo Itigi, Shule ya Sekondari ya Mwanamwema Shein ambayo ipo Kata ya Mgori Wilaya ya Singida na Shule ya Msingi Minyaa iliyopo Kata ya Kinyeto Wilaya ya Singida.

Kesho Dk.Msonde atamalizia ziara yake mkoani hapa kwa kukagua ujenzi wa shule hizo katika Wilaya ya Mkalama na Iramba na kuzungumza na watumishi wa sekta ya elimu na kufanya majumuhisho ya ziara hiyo.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi  ya Rais  Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI (ELIMU) Dk. Charles Msonde, akipanda mti wa kumbukumbu katika viwanja vya Shule Mpya ya Msingi ya Ikungi B wakati wa ziara hiyo.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi  ya Rais  Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI (ELIMU) Dk. Charles Msonde, akikagua ujenzi wa Bweni katika Shule ya Sekondari ya Ikungi. Kushoto ni Mkuu wa Shule hiyo, Neema Stephano na kulia ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Ikungi.
Afisa Elimu Mkoa wa Singida, DK. Elpidius Baganda, akizungumza na walimu na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mwanzi wakati Dk.Msonde alipofika kukagua ujenzi wa madarasa na mabweni unaoendelea katika shule hiyo.
Diwani wa Kata ya Mgori, katika Halmaashauri ya Wilaya ya Singida, Mnyangoi Zuma, akiishukuru Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwapa fedha za ujenzi wa shule mpya ya kidato cha tano na sita.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi  ya Rais  Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI (ELIMU) Dk. Charles Msonde, akisisitiza jambo wakati akizungumza na walimu na wananchi alipokuwa akikagua ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Mwanzi wilayani Manyoni.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi  ya Rais  Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI (ELIMU) Dk. Charles Msonde. akisalimiana na Diwani wa Kata ya Manyoni, Saimon Mapunda.
Afisa Elimu Sekondari Wilaya ya Manyoni, Adelini Mwanisi, akitoa taarifa ya ujenzi wa mradi huo.
Ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa bweni katika Shule ya Sekondari ya Mwanzi ukiendelea. Kulia ni Afisa Elimu Mkoa wa Singida, DK. Elpidius Baganda,
Ukaguzi wa ujenzi wa mabweni hayo ukiendelea.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi  ya Rais  Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI (ELIMU) Dk. Charles Msonde, akitoka kukagua ujenzi wa madarasa katika Shule ya Msingi, Igonoa iliyopo Itigi.
Walimu wa Hamashauri ya Wilaya ya Ikungi wakipongezwa kwa kazi nzuri wanayoifanya.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi  ya Rais  Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI (ELIMU) Dk. Charles Msonde, akimpongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Justice Kijazi kwa kazi nzuri inayofanywa na halmashauri hiyo chini ya uongozi wake.
Muonekano wa ujenzi wa madarasa yanayojengwa Shule ya Sekondari ya Mwanamwema Shein yaliyopo Kata ya Mgori.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi  ya Rais  Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI (ELIMU) Dk. Charles Msonde, akimpongeza Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mwanamwema Shein, Justina Chinemata kwa kazi nzuri anayoifanya ya kusimamia ujenzi wa shule hiyo.
Muonekano wa madarasa yanayojengwa Shule mpya ya Msingi ya Minyaa iliyopo Kata ya Kinyeto Wilaya ya Singida.
 

Share To:

dotto mwaibale

Post A Comment: