Na John Walter-Manyara
Katika picha ni Mbunge wa Babati Vijijini Daniel Sillo akitazama daraja la Mtandaa ambalo limeporomoka na kuwafanya wananchi wa maeneo hayo kupita kwa hofu.
Daraja la Mtandaa lililopo kata ya Kiru wilaya ya Babati mkoani Manyara, ni muhimu kwa kuwa linaunganisha Vijiji vya Kimara,Kiru ndogo na Kiru six na limejengwa kwa miti.
Akiwa katika ziara katika Vijiji vya Kiru ndogo, na Kimara alijionea daraja hilo ambalo lililamikiwa na wananchi na kuahidi kulishughulikia ili huduma za kijamii zipatikane kiurahisi.
Wananchi wamemwambia Mbunge huyo kwamba daraja hilo limeshahatarisha maisha ya wengi hivyo lirekebishwe haraka kuwanusuru.
Post A Comment: