Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinatoa shukurani kwa wapigakura na Watanzania wote kwa ujumla kwa kuendelea kukiamini na kukipatia ushindi wa kishindo katika kata zote 14 zilizofanya uchaguzi mdogo wa madiwani tarehe 13 Julai 2023.


Kata hizo ni Sindeni (Handeni), Potwe (Muheza), Kwashemsi (Korogwe), Bosha (Mkinga), Mahege (Kibiti), Mnavira (Masasi), Magubike (Kilosa), Bunamhala (Bariadi), Ngonywa (Sikonge), Kalola (Uyui), Kinyika (Makete),  Njoro na Kalemawe (Same) na Mbede (Mlele).

Ushindi huu unadhihirisha kukubalika kwa Chama Cha Mapinduzi katika kukidhi matarajio ya kuleta maendeleo kwa wananchi  kupitia  kazi nzuri ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025, inayofanywa na Serikali chini ya uongozi wa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Chama Cha Mapinduzi kinaahidi kuendelea kuwatumikia wananchi kwa uadilifu na uaminifu mkubwa  na kuwa  kiungo madhubuti kati ya  wananchi na serikali kwa maendeleo na ustawi  wa Watanzania.

 

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

 

Sophia Edward Mjema

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa

Itikadi na Uenezi

14 Julai  2023

Share To:

Post A Comment: