Na Denis Chmbi,Tanga.
MWENYEKITI wa chama cha mapinduzi "CCM" Mkoa wa Tanga Rajab Abdurahman amewataka viongozi wa chama hicho pindi wawapo kwenye majukwaa na mikutano ya hadhara ya kisiasa kujibu hoja za wapinzani kwa njia ya amani busara na upole na sio kutumia matuai kejeli wakizidi kudumisha amani na usalama uliopo hapa nchini.
Rai hiyo
ameitoa wakati akiwa kwenye mkutano wake wa hadhara uliofanyika katika
kata ya Msambweni jijini Tanga ambapo amesema kuwa amani na utulivu
vikidumishwa ni nyenzo kubwa ya maendeleo kwa kila mmoja na vikikosekana
huleta machafuko kwa taifa ikiwemo mgawanyiko wa matabaka mbalimbali ya
kisiasa na kidini.
"Unapoona
amani inaendelea kudumu katika nchi yetu na katika mkoa wetu wa Tanga
havijaja kwa bahati mbaya hivi vinakuja kwa mikakati ya maksudi,
tusionyeshe viashiria vya uvunjifu wa amani kwa maneneo na matendo yetu"
"CCM
tunayo mengi sana ya kimaendeleo yaliyofanywa na serikali yakuwaeleza
wananchi kayika sekta mbalimbali Rais wetu anatumia busara na hekima
kuilinda amani ndani ya nchi yetu lakini wenzetu wanatumia nguvu kubwa
kuvunja amani ndani ya nchi yetu" alisema Abdurahman..
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi 'CCM' mkoa wa Tanga Rajab Abdurahman akipandisha bendera ya chama hicho mara baada ya kuzindua tawi jipya la Vatican City lililopo kata ya Msambweni jijini Tanga , tukio lililoanyika july 26,2023.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi 'CCM' mkoa wa Tanga Rajab
Abdurahman (kulia) akicheza mchezo wa draft mara baada ya kuzindua tawi la Umoja wa wanywa kahawa Mabawa lililopo kata ya Msambweni jijini Tanga ,
tukio lililoanyika july 26,2023.
Pamoja
na hayo mwenyekiti huyo amezindua matawi mawili ya chama hicho ndani ya
kata ya Msambweni Vatican City ,Umoja wa wanywa kahawa Mabawaambapo ameagiza mashina na matawi yote yaliyopo ndani
ya mkoa wa Tanga kuhakikisha yanatumika kuiunga mkono serikali katika
mapambano dhidi ya kupiga vita matumizi ya madawa ya kulevya ndoa za
utotoni pamoja na ndoa za jinsia moja.
Akiwa
katika shina la Vatican City Mwenyekiyi huyo amesema kuwa "Shina
liendelee kutumika katika maswala mbalimbali ya kimaendeleo, kusimamia
amani na usalama hususan katika suala la kuiunga mkono serikali katika
maswa la kupiga vita matumizi ya madawa ya kulevya na kupiga vita
maswala ya ndoa za jinsia moja".
Aidha
ameipongeza serikali kutoa fedha katika kutekeleza miradi mbalimbali
mikubwa ya kimaendeleo ndani ya ikiwemo upanuzi wa bandari, ujenzi wa
barabara ya Tanga Pangani yenye urefu wa kilomita 50 ambao umegharimu
kiasi cha shilingi Billion 67 ambao unaendeleo na ujenzi wa daraja kubwa
litakalorahisisha usafiri wa Pangani hadi Bagamoyo pamoja na miradi
mingine katika sekta ya elimu, maji, afya.
"
Sisi watu wa Tanga kwenye miradi ya kimaendelo kutoka january hadi june
2023 tumepewa zaidi ya billion 300 katika ujenzi wa shule, ujenzi wa
miundombinu, afya, na maji, kuna miradi mikubwa ya kimkakati katika
barbara ya Tanga Pangani hadi Bagamoyo kwa kiwango lami lakini kuna
barabara ya kuyoka Handeni mpaka mkoa wa Singida yenye urefu wa Kilomita
384 iliyogharimu zaidi ya Billion 400" alisema Abdurahman.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi 'CCM' mkoa wa Tanga Rajab Abdurahman akipandisha bendera ya chama hicho mara baada ya kuzindua tawi jipya la Vatican City lililopo kata ya Msambweni jijini Tanga , tukio lililoanyika july 26,2023.
Post A Comment: