UONGOZI wa klabu ya Yanga umethibitisha kupokea ofa kutoka Azam FC ya kumuhitaji kiungo wao Feisal Salum (Fei Toto).
Katika taarifa yao kwenda kwa waandishi wa habari, Yanga imeeleza kuwa baada ya mazungumzo ya pande zote mbili na kwa kuzingatia matakwa ya kimkataba kati ya klabu na mchezaji, wamefikia uamuzi wa kumuuza mchezaji huyo.
Taarifa ya Yanga imeeleza kuwa mchezaji huyo ameuzwa kwenda Azam FC kwa dau ambalo halitawekwa wazi kutokana na makubaliano ya pande zote mbili.
Post A Comment: