NA. DENIS CHAMBI,TANGA.
KIONGOZI wa kanisa katoliki Duniani Papa Fransisko amemteua Padre Thomas Kiangio kuwa askofu wa jimbo katoliki la Tanga leo june 7,2023.
Kabla ya uteuzi huo Mhashamu Askofu Thomas John Kiangio alikuwa msimamizi mkuu wa jimbo katoliki la Tanga mara baada ya kufariki kwa aliyekuwa askofu wa jimbo hilo Anthon Mathias Banzi.
Askofu
mteule Thomas John Kiangio wa Jimbo Katoliki la Tanga alizaliwa Machi
17 , 1965 huko Mazinde Ngua wilayani Lishoto, Jimbo Katoliki la Tanga na
lipata malezi na majiundo yake ya Kipadre kutoka Seminari kuu ya
Mtakatifu Antony, Ntungamano Jimbo Katoliki la Bukoba na Karol Lwanga,
Segerea Jimbo Kuu la Dar es Salaam.
Mazoezi
ya Mwaka wa kichungaji aliyafanyia Parokia ya Mlingano, Jimbo Katoliki
la Tanga, akashiriki kwa mwaka mmoja kozi ya Shughuli za kichungaji,
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Mkoani Mwanza. Na ilipotimia tarehe
16 Julai 1997 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre kwa ajili ya Jimbo
Katoliki la Tanga.
Mara
baada ya kupata daraja Takatifu mwaka 1997 Mhasham Askofu Thomas John
Kiangio alieuliwa kuwa mlezi, mwalimu na Gambera Msaidizi na hatimaye
Gambera wa Seminari Ndogo ya Mtakatifu Yosefu Soni, Tanga kati ya mwaka
1998-1999 na kati ya mwaka 2004 hadi mwaka 2013.
Kati
ya mwaka 1999 hadi mwaka 2003 alitumwa kuendelea na masomo ya juu Chuo
kikuu cha Kipapa cha Urbaniana, kilichoko mjini Roma, baadaye kati ya
mwaka 2013 aliteuliwa kuwa Katibu wa Jimbo na kati ya mwaka 2020 hadi
kuteuliwa kwake aliteuliwa kuwa Msimamizi wa Kitume wa Jimbo Katoliki la
Tanga kufuatia kifo cha Askofu Anthony Mathias Banzi aliyefariki dunia
tarehe 20 Desemba 2020.
Post A Comment: