NA DENIS CHAMBI, TANGA.

Waataalam wa kilimo mkoani Tanga wamatakiwa kuvitumia vyena vyama vya ushirikia vilivyopo katika maeneo yao kwa lengo la  kuongeza kasi ya usambazaji wa mbolea za ruzuku zinazotolewa na serikali huku  wenye viti wa vijiji  wakitakiwa  kuwa waaminifu wakati wa kuwasajili wakulima ili kupata idadi sahihi ya  wakulima iliyopo.

Rai hiyo  imetolewa na meneja wa mamalaka ya udhibiti wa mbolea  "TFRA" Kanda ya kaskazini  Gothard Liampawe wakati wa kikao kazi na maafisa kilimo wa ngazi zote na waratibu wa halmashauri zote 11 zilizopo  ndani ya  mkoa wa Tanga na  kwa lengo la kufanya uhamasishaji wa mpango wa serikali wa ruzuku  kuelekea mwaka wa 2023/2024  ikiwa ni lengo la serikali kufanya tahmini kwa mwaka uliopita na namna bora itakayofanyika kuelekea mwaka ujao ili kutimiza adhima ya serikali kupitia sekta ya kilimo.

Alisema kuwa adhima ya serikali ni kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2025 ni kusajili wakulima wapatao zaidi ya million 7 hivyo kuwataka maafisa kilimo wataalamu, waratibu kwa kishirikina na wenye viti wanakwenda kutekeleza kwa pamoja lengo hilo.

"Adhima ya serikali ni kuvitumia vyama vya ushirika kwaajili ya kuongeza usambazaji  wa mbolea lakini pia TFRA kazi yetu ni kutoa magizo kwa wataalam mbalimbali  hivyo nimewaagiza wataalam  mafunzo ambayo tumepeana leo yasiishie hapa waende kule kwa wataalam wa viijiji na kata"

"Lakini pia wale wenye viti naomba wakawe waaminifu wakati wa usajili wa wakulima halisi ambao wako kule kwenye vijiji vyao lakini na wakulima nao nawasisitiza watoe taarifa zilizo sahihi na sisi kama serikali hatutakubali kuona mkulima anatoa taarifa za udanganyifu na watoe taarifa za maeneo wanayo yalima sio  yale amabayo hawayamiliki" alisema Liampawe.

Akizungumza  mdhibiti ubora kutoka TFRA Sheila Yusuph alisema   bado kuna dhana potofu kwa wakulima juu ya mbolea ambazo wanazitumia kwa kushindwa kuzalisha mazao kama walivyotegemea  jambo ambalo limechangiwa na ukosefu wa elimu lakini wao kama mamlaka wanaendelea na akutoa elimu mbalimbali ili kuondoa dhana hiyo.

"Hakuna mbolea ambayo ni mbaya  kikubwa ni elimu tu kwa wakulima  na sisi kama wadhibiti ubora mbolea zote zinazoingia madukani  tumezipima  na  zinapoenda kule madukani zinakuwa na uhakika kwamba mkulima anapoenda kuzitumia  zinaleta mazao yanayotarajiwa lakini cha msingi ni suala tu la elimu kuanzia kule chini kwa maafisa ugani jinsi gani ya kutumia mbolea kwa  kiwango na kwa wakati" alisema Sheila.  

Kwa upande wake afisa kilimo kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Tanga Ayub Mrisho ambaye pia ni mratibu wa zoezi la mbolea za ruzuku kwa halmashauri zote 11 za mkoa alisema kuwa wanaendelea kuhamasisha wakulima kujisajili katika daftali maalum ili kuweza kutambulika kwenye mfumo rasmi kuanzia ngazi vya vijiji . 
 
 

Share To:

Post A Comment: