Na. Damian Kunambi, Njombe
Wanandoa wametakiwa kuacha tabia ya kupekua simu za wenza wao kwakuwa zimekuwa ni chanzo kikubwa cha migogoro ya kifamilia inayopelekea kutoa kwa mauaji ama kusamvaratisha familia.
Hayo ameyasema Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi ambaye pia ni mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto mkoa wa Njombe Wilfred Willa wakati akitoa elimu ya kupinga ukatili katika kijiji cha Matiganjora kilichopo katika Wilaya ya Njombe mkonani humo.
Ameongeza kuwa wanandoa wamekuwa wakifanya doria kwenye simu za wake zao au waume zao na kisha kukutana na vitu vizito ambavyo huwa ni bomu katika ndoa na familia kwa ujumla.
"Wapo ambao wameuana na wengine kuachana katika ndoa kwasababu ya kufanya doria kwenye simu za wenza wao kufanya hivi kunaleta madhara makubwa hivyo kama hakuna umuhimu wa kuipekua ni vyema kuachana nayo basi kwa maslahi ya ndoa yako na familia.
Sanjari na hilo pia amewataka wazazi kukaa na watoto kwa ukaribu katika kipindi hiki cha likizo ili wasipate mazingira ya kufanyiwa ukatili hasa ubakaji na ulawiti.
Post A Comment: