Katika kukabiliana na Migogoro baina ya wawekezaji na wananchi , Mbunge WA Jimbo la monduli mh Fredrick lowassa amewataka wawekezaji kujenga mahusiano mazuri ya kijirani na wananchi Wa maeneo yanayo wekeza kwa kwa kushirikiana na kuvumilia pale panapotokea kasoro.

Ametoa wito huo wakati akizindua mradi wa maji Utakaonufaisha Vitongoji vitatu, Silongoi, Nongai, kilimatinde chini, wenye watu zaidi ya Elfu mbili (2),katika Kijiji Cha kilimatinde kata ya moita wilayani monduli ulio kabidhiwa na mwekezaji wa kampuni ya Arusha art bwana Atesh ambae amewajengea wananchi wa eneo Hilo mradi huo ulio gharimu zaidi ya shilingi ml.30 za kitanzania, kwa kushirikiana na Nguvu KAZI za wananchi wa Eneo Hilo.

Mhe. Fredrick amemshukuru mwekezaji huyo na kuwataka wawekezaji wengine wanaowekeza katika Maeneo ya Jamii ya kifugaji monduli, Kwa kuwasaidia Maji kutokana na hitaji Hilo kuwa kubwa katika jamii hiyo huku akisisitiza swala la mahusiano mazuri na Wana monduli.

Kwa upande wake mkurugenzi huyo Wa kampuni ya Arusha Art amewashukuru wananchi WA Kijiji hicho Kwa kuupokea mradi huo na kuahidi kuendelea kushirikiana nao katika  swala la elimu na kuahidi kujenga madarasa mawili, katika Kijiji hicho.



Share To:

Post A Comment: