Wawakilishi wa wanawake wafanyakazi wa mgodi wa Barrick Buzwagi wakikata keki wakati wa hafla hiyo.
Dkt. Martha Jotham akitoa neno fupi kwa wanawake wanaofanya kazi katika mgodi wa Buzwagi na kuwatia moyo wa kuendelea kupenda kazi yao.
Mhandisi Zonnastraal Mumbi (PEng), akiongea akifungua hafla hiyo ya wanawake wafanyakazi wa mgodi wa Buzwagi
Mhandisi Zonnastraal Mumbi (P Eng) Akikabidhi zawadi kwa baadhi ya wafanyakazi katika hafla hiyo.
Wanawake wafanyakazi wa mgodi wa Barrick Buzwagi wakifurahi pamoja wakati wa hafla hiyo.
Wanawake wafanyakazi wa mgodi wa Barrick Buzwagi wakifurahi pamoja wakati wa hafla hiyo.
Wanawake wafanyakazi wa mgodi wa Barrick Buzwagi wakifurahi pamoja wakati wa hafla hiyo.
***

Wanawake nchini wametakiwa kujitokeza kuchangamkia fursa za kufanya kazi migodini badala ya kuamini kuwa kazi za migodini na sekta ya madini kwa ujumla ni za wanaume.


Wito huo umetolewa wakati wa hafla ya usiku wa wanawake wanaofanya kazi katika mgodi wa Barrick Buzwagi, uliopo Kahama mkoani Shinyanga ambapo upo katika mchakato wa kufungwa.

Akifungua hafla hiyo,Mwakilishi wa Meneja Mkuu wa mgodi wa Barrick Buzwagi,Mhandisi Zonnastraal Mumbi (PEng), alisema hafla hiyo ni ya kusherehekea na kuwapongeza wanawake wote wanaofanya kazi katika mgodi huo na kuwatia moyo wa kuendelea kujiamini zaidi.

Mgeni rasmi katika hafla hiyo, Dkt. Martha Jotham, ambaye ni Mtawala na Mkufunzi wa Taasisi ya Biblia duniani (WIBI) ya Mkoani wa Mwanza, aliwataka wanawake nchini kuchangamkia fursa zilizopo katika sekta ya uchimbaji wa madini na alipongeza jitihada zinazofanywa na Mgodi wa Buzwagi kwa kutambua mchango wa wanawake katika mgodi .

Dkt, Jotham alitoa rai kwa Wanawake hao kutambua kuwa wao ni wa thamani na wa pekee pamoja na kuwa wanafanya kazi ngumu na wanakutana na changamoto nyingi wanatakiwa kujiamini kwa kile wanacho kifanya ndiyo maana mgodi unatambua jitihada zao katika utendaji kazi wao na ndiyo maana wameandaliwa hafla hii.

Aliwashauri kuwa mambo ya msingi wanayopaswa kuyazingatia wanapokuwa kazini ni kujitambua kwa kuchapa kazi kwa bidii, kujipenda kwa kuhakikisha wanavaa vizuri na kula vizuri na kujiwekea akiba kutokana na kipato chao kwa ajili ya kuwasaidia katika siku za mbele.

Dkt. Jotham, aliwataka kumtanguliza Mungu mbele katika kazi zao, kujiamini na kuthubutu wa kutenda mipango ya maendeleo ya jamii waweke mikakati na mipango yao vizuri wakitabua maisha yao hayahitaji mtu mwingine,maisha yao yanawahitaji wao.

Katika hafla hiyo pia wanawake wa mgodi huo walizawadiwa zawadi mbalimbali.

Share To:

OKULY BLOG

Post A Comment: