NA DENIS CHAMBI, TANGA.
Wakala wa vipimo Tanzania ‘WMA’ mkoa wa Tanga imewataka wauzaji na wasambazaji wa mitungi ya gas ya kupikia ya jumla na reja reja kuhakikisha kuwa ujazo wa mitungi wanayowauzia wananchi inakuwa sahihi na kuepukana na udanganyifu wa aina yeyote ile ili kujipatia faida zaidi kinyume cha sheria na taratibu zilizowekwa.
Wito
huo umetolewa na Afisa mwandamizi wa wakala wa vipimo Tanzania ‘WMA’
mkoa wa Tanga Ally Mtowa wakati akizungumza na waandishi wa habari
kwenye maonyesho ya 10 ya biashara na utalii yanayoendelea katika
viwanja vya Mwahako ambapo alisema katika kuwadhibiti wauaji wote wa
mitungi ya gas ofisi hiyo imekuwa na utaratibu wa kutoa elimu kwa
wafanyabaishara wote.
“Tumeshafanya
semina kwa wadau ambao wanafanya biashara za kuuza gas wakiwemo wale
wanaojaza mitungi viwandani pamoja na wale wauzaji wa jumla na reja
reja wamepewa elimu ya namna gani wahakikishe mitungi inakuwa na ujazo
sahihi na anatakiwa wawe na mzani ambao umehakikiwa na wakala wa vipimo
na apime ule mtungi wa gas kama una ujazo sahihi kabla hajaanza
kumuuzia mwananchi”
Aidha
amewataka wafanyabiashara na wamiliki wa vituo vya mafuta kutokuchezea
mizani wakati wa kuwahudumia wateja akisema kuwa yapo baadhi ya
malalamiko kutoka kwa wateja wakiwemo wamiliki na madereva wa vyombo
vya usafiri wakilalamika juu ya changamoto hiyo ambayo inaenda kinyume
cha sheria zilizowekwa .
Hata
hivyo Mtowa alisema katika kutua changamoto licha ya kuendelea
kuwabana na kuwachukulia sheria wamiliki na wafanya biashara wa vituo
vya mafuta ofisi ya wakala wa vipimo mkoa wa Tanga imekuwa ikitoa elimu
kwa wananchi mara kwa mara ili kuwa na uelewa pale wanapoenda kupata
huduma hiyo huku akiwataka kutoa taarifa pindi wanapo baini udanganyifu
wa aina yeyot.
“Majukumu
yetu zaidi ni kumlinda mlaji na madhara yatokanayo na vipimo ambavo
havina usahihi mfano katika vituo vya kujazia mafuta tunahakikisha
kipimo kinatoa mafuta kwa usahihi sheria zipo ambazo zinawaongoza na
kuwabana wamiliki na wafanyabiashara wote wanaouza mafuta wapo ambao
tumeshawachukulia hatua ikiwemo kupigwa faini na kama kosa litajirudia
rudia wanaweza kufikishwa mahakamani , nawaomba wawe waadilifu kuweza
kuhudumia wananchi na wahakikishe kwamba muda wote vipimo vyao vinakuwa
sahihi” alisema afisa huyo.
Pamoja
na hayo alisistiza zaidi kwa wafanyabiashara wadogo wadogo wanaouza
vyakula na vitu vya majumbani kuhakikisha kuwa mizani zao wanazotumia
kupimia zinakuwa na ubora na zilizo hakikiwa n a ofisi ya wakala wa
vipimo kadiri ya utaratibu uliowekwa hii ikilenga kutoa huduma zaidi kwa
wananchi na kuwalinda na madhara ambayo yanaweza kujitokeza.
“Tumekuwa
tukitoa elimu mara kwa mara kwa wananchi kwahiyo tunajitahidi kwa kiasi
kikubwa kuhakikisha kwamba tunamlinda mwananchi kwenye vipimo , tuna
kaguzi za m iani ambazo zinafanywa na watendaji katika serikali za mitaa
lakini na wao wafanyabishara wenyewe tunawaelimisha jinsi ya kutumia
mizani na kama ni mwananchi wa kawaida uzingatia vitu gani na pindi
unapoona kuna udanganyifu wa vipimo usisite kufika ofisni ili tuweze
kuchukua hatua zaidi” aliongeza.
Maonyesho
ya biashara na utalii ambayo hufanyika kila mwaka jijini Tanga
yakihusisha makampuni na taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali
mwaka huu yakiwa ni ya 10 yamebebwa na kauli mbiu ya ‘Kilimo , viwanda
utalii na madini ndio msingi wa maendeleo ya kiuchumi’
Post A Comment: