NA DENIS CHAMBI, TANGA.
JESHI
la Polisi mkoa wa Tanga katika kukabiliana na uhalifu ,wahalifu pamoja
na kupiga vita matumizi ya madawa ya kulevya limekuja na michauano ya
mpira wa miguu kwa vijana waliopo ndani ya halmashauri ya jiji la Tanga
inayotarajiwa kuanza kurindima ifikapo July 8, 2023.
Michauano
hiyo inayotarajiwa kuzihusisha zaidi ya timu 20 kutoka katika mitaaa ya
viunga vya jiji la Tanga ambapo itachezwa kwa mfumo wa mtoano na kwa
upande wa zawadi mbalimbali zitatangazwa hapo baadaye kwa bingwa wa
mwaka huu 2023 pamoja na washindi wengine.
Akizungumza
wakati wa kikao cha pamoja na wawakilishi wakiwemo viongozi wa timu
zitakazo shiriki michauano hiyo kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa
Tanga Henry Mwaibambe amesema wamelenga kupitia mashindano hayo ujumbe
wa kupinga na kupiga Vita matumizi ya madawa ya kulevya umfikie kila
mmoja popote pale alipo ili kizazi kijacho kiwe salama na kishiriki
katika ujenzi wa Taifa
Aidha
alisema pamoja na kupiga vita matumizi ya madawa ya kulevya ni wajibu
wa kila raia kuhakikisha anashiriki kikamilifu katika masuala mazima ya
ulinzi na usalama wakishirikiana na vyombo vya dola katika kuwabaini
wale wote wanaovunja sheria na waharifu
"
Mimi ni muumini sana wa usalama na lengo letu sisi hapa sote ni
kwaajili ya usalama wetu, usalama wa maisha ya mwanadamu ndio kila kitu
duniani athari za uhalifu zinaweza kumkuta yeyote yule na mahali popote
hivyo naomba sana kupitia mashindano haya tushirikiane kuwabaini
wahalifu"
Akizungumza
Polis jamii Frank Kipengele alisema ili kupata madhumuni na malengo ya
ligi hiyo itachezwa mtaa husika wenye kila timu ili kuweza kuwafikia
walengwa ambao ni wananchi na itakapofika siku ya fainali watachagua
uwanja wenye watu wengi.
"Kwenye
mechi ya ufunguzi tutatafuta kiwanja ambacho tutakiona kitakuwa na
washiriki wengi na kitakuwa na watu wengi sana ambao tutaweza kuongeza
nao kwenye siku ya ufunguzi na viongozi tutawajulisha lakini kwa mechi
nyingine tutazipanga kwenye viwanja ambavyo timu husika zinatoka na
wala sii sehemu nyingine zozote "
"
Utaratibu wa mashindano utakuwa ni wa mtoano mpaka tunafika robo
fainali Kwenye fainali pia tutatafuta kiwanja ambacho kitakuwa na watu
wengi kwaaajili ya kutangaza adhima ya mashindano haya na kuhusu
kiingilio tutakaa na viongozi tim husika tunafanya viingilio ili timu
zione thamani ya mashindano haya" alisema Kipengele
Post A Comment: