Mbunge wa Jimbo la Monduli Fredrick Lowassa Amewataka Wananchi kuendelea kuwa na Imani na Serikali ya Awamu ya Sita katika Uwekezaji wa Miradi ya Maendeleo.
Mheshimiwa Fredrick Lowassa ameyasema katika Harambee ya Ujenzi wa Kituo Cha Afya kata ya Sepeko Akimwakilisha Mgeni Rasmi Ambaye alitarajiwa kufika hapo Waziri wa Madini DOTTO BITEKO, Ambapo jumla ya Fedha zilizopatikana ni Millioni 248.
"Jumatatu mapema tutakuwa Bungeni kwa ajili ya kupitisha bajeti kuu ya Serikali Kila mbunge atachagua jibu Moja ndiyo au Hapana, kupitia hili Leo na Mhadhara huu mnataka nikaseme ndiyo au Hapana?"
"Sasa kama jibu ni ndiyo ,kule bungeni ndo majeti inavyopitishwa hivyo, bunge Lina vyanzo vyake vya mapato na Kuna swala la Bandari ya nchi yetu linaendelea katika mitandao ya kijamii, unaambiwa kama ni mwanasiasa kimbia mjadala huu, lakini kama wewe ni mwakilishi wa wananchi lazima niseme neno, NAMI Nina neno Moja kama huu mkataba una baraka za Mama Samia,Mimi ni nani nisimwamini ,miradi mingi ambazo ametuletea hatujui hata chanzo chake ni nini,Kwa hiyo hata ukiona mjadala huu unaendelea tafakari ya kwako, tafakari ya Monduli msishabikie Mimi mbunge wenu Namuamini Rais kwa asilimia 100%".
Kufuatia Risala iliyosomwa , Mradi wa ujenzi wa kituo hicho Cha Afya ulianza mwaka 2020 kwa nguvu za Wananchi lakini baadaye kusimama kutokana na ukosefu wa Mapato , huku ikielezwa kuwa mradi huo endapo utakamilika itahudumia Taasisi mbalimbali katika kata hiyo wenye Takriban watu elfu 25, na itahudumia pia kata za Jirani kama Lepurko na Makuyuni .
Post A Comment: