NA DENIS CHAMBI, TANGA.
MAMLAKA ya Usimamizi wa Wanyama pori Tanzania 'TAWA' imewaomba waandaaji na maonyesho ya biashara na utalii Tanga ambao ni chemba ya biashara 'TCIAA' kuendelea kuboresha mazingira yatakayosaidia na kuwavutia wafanyabiashara, wawekezaji, taasisi , makumpuni , wajasiriamali mbalimbali na wananchi kwa ujumla na hatimaye kuweza kushiriki kwa wingi maonyesho hayo ambayo hufanyika kila mwaka katika viwanja Mwahako.
Ombi
hilo limetolewa na afisa mhifadhi mwandamizi kutoka mamlaka ya
Usimamizi wa Wanyama pori Tanzania 'TAWA' Proches Rongoma mara baada ya
kufungwa rasmi kwa maonyesho ya 10 biashara na utalii yaliyofanyika kwa
siku 10 katika viwanja vya Mwahako jijini Tanga na mkuu wa mkoa huo
Waziri Kindamba June 6, 2023.
Rongoma
alisema kuwa idadi ya watalii na wananchi waliojitokeza kuangalia
wanamnayama mbalimbali katika bustani iliyopo kwenye viwanja hivyo
haikuwa kubwa kama ilivyotarajiwa hii ni kutokana na hali ya hewa
ambapo mvua zilinyesha kwa wingi hivyo kupelekea washiriki wengi
kushindwa kufika katika maonyesho hayo.
"Tuliwaambia
waandaaji wa maonyesho ya biashara na utalii ambayo ni chemba ya
biashara Tanga kutengeneza mradi wa kudumu ambao utaonekana kama maeneo
mengine ya maonyesho, kutengeneza mazingira yote ya maonyesho kila banda
ili kuweza kuwavutia watalii na wafanyabiashara wengi zaidi kwa
maonyesho yajayo"
"Maeneo
ya mabanda yajengwe katika namna ambayo yatapauliwa na mabati ili
yasiharibike mapema yawe ya kudumu tunategemea kwamba wataweza
kuboresha eneo hili hasa kunapokuwa na mvua nyakati zote kwa sababu
ukiangalia kwa mwaka huu mvua zimeathiri sana tumekosa watalii wengi
zaidi ya vile ambavyo tulitegemea" alisema Rongoma.
Akizungumzia
maonyesho hayo ya biashara na utalii ya 10 kufanyika jijini Tanga Afisa
huyo alisema kuwa kila mwaka TAWA wamekuwa wakiyaboresha kwa kuongeza
wanyama pori na ndege wa aina tofauti tofauti hii ikilenga zaidi
kuwavutia watalii wa ndani na hatimaye kutembelea hifadhi mbalimbali
zilizopo hapa nchini.
"Maonyesho
ya mwaka 2023 yamekwenda kwa namna ya tofauti zaidi kwa upande wetu
TAWA tuliyaboresha kwa kuwaletea Wanyama pori na ndege wa tofauti
tofauti na wananchi waliotembelea maeneo haya na kuwaona wanyama na
ndege na wamefurahia kuwaona na hiyo yote ni kwaajili ya kuzitangaza
hifadhi za Tanzania" aliongeza.
Kwa
upande wake Afisa mhifadhi daraja la pili kutoka Mamlaka ya usimamizi wa wanyama
pori Tanzania TAWA Veronica Mollel amesema ushiriki wao wa kila mwaka
katika maonyesho hayo umekuwa na mchango mkubwa katika kuzitangaza
hifadhi za Tanzania ambapo wananchi wengi na wadau wamehamasika na
kuweza kuzitembelea mbuga mbalimbali zilizopo.
"Ushiriki
wetu katika maonyesho haya ya biashara na utalii yanayofanyika kila
mwaka hapa jijini Tanga umekuwa na tija sana kwa jamii wananchi wengi
wamekuwa wakihamasika ukiangalia asilimia kubwa waliokuwa wanakuja
katika maonyesho haya waliokuwa wanakuja kuona wanyama kwahiyo sisi
Kama TAWA kuwepo hapa tumehamasisha watalii wengi zaidi kuzitembelea
hifadhi na mbunga mbalimbali zilizopo"
Aliongeza
kuwa kila mwananchi au taasisi inaturusiwa kujenga vitalu na bustani
za kufugia wanyama wa aina tofauti tofauti isipokuwa kwa kufuata sheria
ambazo ni pamoja na kuwa na leseni ya biashara eneo lenye vigezo
vinavyokidhi.
Yasin
Mndeme ambaye ni mmoja wa wananchi waliojitokeza katika maonyesho hayo
pamoja na kufanya utalii wa ndani katika bustani ya wanyama pori na
ndege alisema ni kuwaona fahari kwao kuwaona wanyama ambao ni adimu
hivyo kuiomba serikali pamoja na waandaaji wa maonyesho hayo kuangalia
namna ya kuweza kuongeza siku ikiwezekana kufanyika mara mbili kwa
mwaka.
Afisa mhifadhi mwandamizi kutoka mamlaka ya
Usimamizi wa Wanyama pori Tanzania 'TAWA' Proches Rongoma akitoa maelezo kwa mkuu wa mkoa wa Tanga Waziri Kindamba (wa kwanza kulia ) kuhusu utendaji wa mamlaka hiyo wakati wa kufunga maonyesho ya 10 ya biashara na utalii yaliyofanyia katika viwanja vya Mwahako, wa kwanza kulia ni mwenyekiti wa chemba ya biashara (TCIAA) mkoa wa Tanga Rashid Mwanyoka.
Baadhi ya wanachi na wakazi wa jiji la Tanga wakiangalia wanyama waliopo kwenye vitalu vilivyowekwa na mamlaka ya usimamizi wa wanyama pori TAWA kwenye maonyesho ya biashara na utalii.
Post A Comment: