NA DENIS CHAMBI, TANGA.
MAMLAKA
ya usimamizi wa wanyama pori Tanzania 'TAWA' imewataka wananchi waliopo
karibu na hifadhi za wanyama kujiepusha na vitendo vyovyote vya
ujangiri wa wanyama katika hifadhi na maeneo mbalimbali hapa nchini
huku matukio ya ujangiri yakielezwa kupungua kwa sasa hii ikichangiwa na
Elimu iliyokuwa ikitolewa.
Rai
hiyo imetolewa na Ofisa Mhifadhi mwandamizi kutoka Mamlaka ya Usimamizi
wa Wanyama pori Tanzania 'TAWA' Proches Rongoma wakati wakishiriki
maonyesho ya 10 ya Biashara na Utalii yanayofanyika mkoani Tanga kila
mwaka ambapo amesema kuwa hivi karibuni waziri wa Mali asili na Utalii
Mohammed Mchengerwa alizindua mpango kabambe utakaosaidia kwa kiasi
kikubwa kuwadhibiti wale wote waliokuwa wakikiuka sheria za kuuwa
wanyama pori bila kibali maalum.
"Suala
au kitendo chochote cha kuuchukua mali ya wanyama pori bila kibali huo
ni ujangiri na ujangiri upo wa aina tofauti upo wa kibiashara na wa
chakula kuna watu wanao uwa wanyama kwa ajili ya chakula na kwaajili ya
kufanya Biashara mamlaka ya wanyama pori Tanzania inapenda kuwasihi
Sana watanzania wajue kwamba wao ndio wahifadhi wa kwanza wa wanyama
pori wa nchi hii"
"Serikali
yetu imeleta mfumo wa kupatikana kwa nyama za wanayama. pori katika
bucha kwahiyo hakuna sababu ya kusema mtu anawinda ili apate kitoweo
kwahiyo tuna mfumo unaokubalika ambao unakuruhusu vinginevyo utakutwa na
mkono wa Sheria hivyo Ni vyema watanzania wajiepushe na ujangiri wa
aina yeyote ile" alisema Rongoma
Aidha
aliwataka Wananchi wanaoishi karibu na hifadhi mbalimbali hapa nchini
kutoa taarifa kwenye Mamlaka husika na kujiepusha kujichukulia hatua
mkononi pale wanyama pori wanapokuwa wamevamia katika maeneo ya shughuli
za kibinadamu,
"Yapo
baadhi ya maeneo yenye changamoto za Wanyama pori kutoka hifadhi
mbalimbali kutoka nje ya hifadhi na kwenda kuvamia maeneo ya shughuli za
kibinadamu Kama kilimo na makazi , ninachoomba Wananchi mnapoona
wanyama pori msiwasogelee karibu na msichukue hatua mkononi ni hatari
Sana nivyema mkatoa taarifa kwenye Mamlaka husika"alisisitiza Rongoma
Awali
akizungumza afisa mhifadhi daraja la pili kutoka Mamlaka hiyo Veronica
Mollel aliwasisitiza na kuwahimiza watanzania kuendelea kufanya utalii
wa ndani katika hifadhi mbalimbali zilizopo hapa nchini ili kujionea
vivutio na kujifunza amali mbalimbali zilizopo.
Alisema
kuwa kuzinduliwa kwa Royal Tour iliuofanywa na Rais wa jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kumekuwa na muamko mkubwa wa
watalii sii tu wageni kutoka mataifa mbalimbali bali hata watanzania
wamehamasika na kujitokeza kujionea vivutio huku ushiriki wa wanawake
katika sekta mbalimbali ukiongezeka.
"Tanzania
tuna vivutio mbalimbali ushiriki wa wanawake katika sekta mbalimbali
za utalii umekuwa ni mkubwa wapo kwenye doria, kuongoza watalii
niwasihi watanzania wote kuwa mabalozi wa rasilimali zetu za Wanyama
pori" alisema Mollel.
Maonyesho
ya biashara na utalii ambayo hufanyika kila mwaka mkoani Tanga
yakishitikisha makampuni, taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali
mwaka huu 2023 yamebebwa na kauli mbiu ya "Kilimo, viwanda utalii na
madini ndio msingi wa maendeleo ya kiuchumi"
Baadhi ya wanachi wa jiji la Tanga waliojitokeza katika maonyesho ya biashara na utalii yanayofanyika katika viwanja vya Mwahako wakiangalia baadhi ya wanyama wanaopatikana katika hifadhi mbalimbali hapa nchini wakiwa wapo kwenye mabanda ya maonyesho hayo.
Post A Comment: