Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Taasisi ya Flaviana Matata Foundation leo imekabidhi mradi wa vyoo viwili vyenye matundu 24 katika Shule ya sekeondari Mazinge iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga vyenye thaman ya shilingi milioni 58 kama hatua ya kuunga mkono juhudi za serikali.

Akizungumza Meneja miradi wa taasisi ya Flaviana Matata Foundation Lineth Masala amesema mradi huo umelenga kuondoa changamoto ya upungufu wa matundu ya vyoo katika shule hiyo.

Amesema mradi huo umeanza kutekelezwa Mwezi Machi Mwaka huu 2023 ambapo umekamilika Mwezi Julai 2023 na kwamba taasisi ya Flaviana Matata Foundation inatekeleza miradi kupitia ufadhili wa Diamonds do good.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi vyoo hivyo mkurugenzi wa taasisi ya Flaviana Matata Foundation amesisitiza walimu na wanafunzi wa shule hiyo kutunza miundombinu ya mradi huo ili uweze kudumu na kuendelea kuwanufaisha.

Flaviana Matata ameisihi jamii kuacha mila potovu ambapo amewaomba wazazi kutimiza wajibu wao katika malezi bora kwa watoto huku akiwasisitiza wanafunzi kusoma kwa bidii ili waweze kutimiza ndoto zao.

“Tunamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan tunaamini hivi tunavyovifanya kwa kushirikiana na serikali vitaenda kutatua changamoto zilizopo wazazi mpo walimu na wanafunzi niwaombe tuvunje mila potovu tuwaache watoto wa kike wasome tuache mimba na ndoa za utotoni hivi vyoo tumejenga kwa lengo la kutatua changamoto zilizokuwepo”

“Sisi tumejikita kuhakikisha tunatatua changamoto zinazomkabili mtoto wa kike ili aweze kupata elimu na kujikwamua kiuchumi na sisi tutaendelea kushirikiana na ninyi siku zote lakini niwaombe mvitunze ili vije kutumiwe na wadogo zenu wanaofuata na viongozi mtusaidia kutunza miundombinu lakini pia tutafurahi kuona matokea ufaulu unaongezeka”. Amesema Flaviana Matata

Kwa upande wake mgani rasmi kwenye hafla hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi ameipongeza taasisi ya Flaviana Matata Foundation kwa kutatua changamoto ya vyoo katika shule ya sekondari Mazinge ambapo amesisitiza wanafunzi kuongeza juhudi katika masomo ili kuwatia moyo wadau wa maendeleo wanaowekeza mazingira bora na salama.

“Niipongeze sana taasisi ya Flaviana Matata Foundation kwa kukabidhi mradi huu leo lakini  Mradi huu ambao umeletwa na taasisi ya Flaviana Matata Foundation wanafunzi wa shule ya sekondari Mazinge ni wanufaika wa moja kwa moja tunaamini mazingira haya yatasaidia kuongeza ufaulu darasani hasa kwa watoto wa kike ambao kipindi cha nyumba mlikuwa mnashindwa kufika shuleni, niwaombe wanafunzi wote mtumie vyoo hivi kama ilivyokusudiwa ili uweze kuishi miaka mingi tusiharibu miundombinu”.amesema DC Samizi

Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Dkt. Jomaary Satura naye ameipongeza taasisi ya Flaviana Matata Foundation kwa kuendelea kuisaidia serikali kutatua changamoto zilizopo ambapo amesema   serikali Manispaa hiyo itaendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo kwa kuruhusu uwekezaji hasa katika sekta ya elimu.

Naye Mkuu wa Shule ya sekondari Mazinge  Mwalimu James Msimba amesema vyoo hivyo vitakuwa ni chachu ya kuongeza ufaulu kwa wanafunzi na kwamba ameishukuru taasisi ya Flaviana Matata Foundation huku akiomba kuendelea kushirikiana katika kutatua changamoto zingine zilizopo.

“Uongozi na jumuiya ya shule ya sekondari Mazinge tunaishukuru serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi shupavu wa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira salama kwa taasisi mbalimbali zisizo za kiserikali”

“Tunaishukuru taasisi ya Flaviana Matata Foundation kwa msaada wao wa kutujengea matundu 24 ya vyoo pia kwa msaada wa taulo za kike ambazo walitoa kwa wanafunzi wa kike 135 katika shule yetu Mungu awabariki sana kwa moyo wenu wa majitoleo na upendo”.amesema Mwalimu James mkuu wa shule

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Mazinge wamesema vyoo hivyo vitawasaidia kuondokana na changamoto zilizokuwa zinawakabili hasa kwa wanafunzi wa kike.

Taasisi ya Flaviana Matata Foundation leo Juni mosi,2023 imekabidhi vyoo viwili vyenye matundu 24 ambavyo vina thaman ya shilingi milioni 58 kama hatua ya kuunga mkono juhudi za serikali katika Shule ya sekeondari Mazinge iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga

Mkurugenzi wa taasisi ya Flaviana Matata Foundation, Flaviana Mtata akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi vyoo ya kisasa katika shule ya sekondari Mazinge Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga leo Juni mosi 2023.

Mkurugenzi wa taasisi ya Flaviana Matata Foundation, Flaviana Mtata akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi vyoo ya kisasa katika shule ya sekondari Mazinge Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga leo Juni mosi 2023.

Mkurugenzi wa taasisi ya Flaviana Matata Foundation, Flaviana Mtata akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi vyoo ya kisasa katika shule ya sekondari Mazinge Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga leo Juni mosi 2023.

Mgeni rasmi, mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza kwenye hafla iliyoratibiwa na taasisi ya Flaviana Matata Foundation kwa ajili ya kukabidhi mradi wa matundu ya vyoo leo Juni mosi 2023 katika shule ya sekondari Mazinge Manispaa ya Shinyanga.

Mgeni rasmi, mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza kwenye hafla iliyoratibiwa na taasisi ya Flaviana Matata Foundation kwa ajili ya kukabidhi mradi wa matundu ya vyoo yenye thamani ya shilingi milioni 58 katika shule ya sekondari Mazinge Manispaa ya Shinyanga.

Mkurugenzi wa taasisi ya Flaviana Matata Foundation, Flaviana Mtata upande wa kushoto na Mgeni rasmi, mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi wakiteta jambo kwenye hafla ya kukabidhi vyoo vya kisasa shule ya sekondari Mazinge Manispaa ya Shinyanga.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Dkt. Jomaary Satura akizungumza kwenye hafla iliyoratibiwa na taasisi ya Flaviana Matata Foundation kwa ajili ya kukabidhi mradi wa matundu ya vyoo yenye thamani ya shilingi milioni 58 leo katika shule ya sekondari Mazinge.

Meneja miradi wa taasisi ya Flaviana Matata Foundation Lineth Masala akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi mradi wa matundu ya vyoo leo Juni mosi 2023 katika shule ya sekondari Mazinge Manispaa ya Shinyanga.

Mkuu wa Shule ya sekondari Mazinge  Mwalimu James Msimba akisoma taarifa ya shule kwa mgeni rasmi katika hafla ya kupokea mradi wa matundu ya vyoo 24 yenye thamani ya shilingi milioni 58.





Share To:

Misalaba

Post A Comment: