Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Kampeni ya Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii
Tanzania SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na maafisa ustawi wa jamii
wametoa elimu ya ukatili kwa wanafunzi wa timu ya UMISETA Mkoa wa Shinyanga
ambao wapo kwenye kambi katika chuo cha ualimu SHYCOM.
SMAUJATA ni kampeni ya kitaifa ya kupinga ukatili wa kijinsia Nchini Tanzania iliyoanzishwa mwaka 2022 chini ya wizara ya maendeleo ya jamii,
jinsia, wanawake na makundi maalumu ambayo inayosimamiwa na Waziri Dkt.
Dorothy Gwajima.
Mwenyekiti wa SMAUJATA Mkoa wa
Shinyanga Bi. Nabila Kisendi jina maarufu Madam Kisendi emetoa elimu ya ukatili
kwa wanafunzi hao huku akiwasisitiza kuvunja ukimya kwa kutoa taarifa za
ukatili unaoendelea kufanyika katika jamii hasa wawapo shuleni ili kutokomeza
vitendo hivyo.
Madam Kisendi ametaja aina mbalimbali
za ukatili ikiwemo ukatili wa kijinsia pamoja na ukatili wa kingono ambapo amewasihi
wanafunzi hao kuepuka ukatili na kwamba amewasisitiza kusoma kwa bidii ili waweze
kutimiza malengo yao.
“Kuna ukatili wa kimwili unafanyika huko shuleni ninyi
msikubali kufanyiwa lakini pia ukatili wa kijinsia msikubali haya yafanyike
mkiona mtoto anafanyiwa vitendo vya ukatili toa taarifa au piga simu namba ya
bure kabisa ya serikali ambayo ni 116 lakini kuna viongozi wa vijiji, mitaa
watendaji na maafisa ustawi wa jamii mtoe huko taarifa”.
“Kwa umri wetu huu mnatakiwi kusoma kwa bidii ili mtimize
ndoto zenu achana na huu ukatili wa kingono utapata ujauzito na hizi ni mimba
za utotoni ambazo zinakatisha malengo ya watu wengi kwahiyo msifanye mapenzi
mkiwa na umri mdogo someni kwanza hayo mambo kuna wakati wake”.amesema Mwenyekiti Madam Kisendi
Katika hatua nyingine afisa ustawi wa
jamii wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Bi. Ansila Materu amesema
serikali itaendelea kuchukua hatua kali kwa wale wanaofanya vitendo vya ukatili
kwa watoto ikiwemo ubakaji na ulawiti ambapo
amewasisitiza wanafunzi hao kuendelea kuzingatia taratibu na miongozi zilizopo
shuleni ili waweze kumaliza masomo yao salama.
Aidha baadhi ya viongozi wa SMAUJATA
Mkoa wa Shinyanga akiwemo makamu mwenyekiti wa kampeni hiyo Mkoa wa Shinyanga
Mwalimu Vicent Kanyogota nao wametoa
elimu juu ya ukatili kwa wanafunzi wa timu ya UMISETA Mkoa wa Shinyanya.
Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi wa
timu ya UMISETA Mkoa wa Shinyanga wameshukuru na kuwapongeza viongozi wa
kampeni ya SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga kwa kutoa elimu hiyo ambapo wameahidi
kuwa mabalozi wazuri wa kupinga ukatili hasa wawapo shuleni.
Nao baadhi ya walimu na walezi wa
wanafunzi wa timu ya UMISETA Mkoa wa Shinyanga wamepongeza kwa elimu hiyo huku
wakiwaomba viongozi wa kampeni ya SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga na maafisa ustawi
wa jamii kuendelea kutoa elimu hiyo ya ukatili kwenye shule mbalimbali ili
kudhibiti ukatili wanaofanyiwa wanafunzi aidha bila wao kujua.
Mwenyekiti wa SMAUJATA Mkoa wa
Shinyanga Bi. Nabila Kisendi jina maarufu Madam Kisendi akitoa elimu ya ukatili
kwa wanafunzi wa timu ya UMISETA Mkoa wa Shinyanga waliopo kambi katika chuo
cha ualimu SHYCOM, leo Jumatatu Juni 12,2023.
Mwenyekiti wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Bi. Nabila Kisendi jina maarufu Madam Kisendi akitoa elimu ya ukatili kwa wanafunzi wa timu ya UMISETA Mkoa wa Shinyanga waliopo kambi katika chuo cha ualimu SHYCOM, leo Jumatatu Juni 12,2023.
Afisa ustawi wa jamii wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Bi. Ansila Materu akitoa elimu ya ukatili kwa wanafunzi wa timu ya UMISETA Mkoa wa Shinyanga waliopo kambi katika chuo cha ualimu SHYCOM, leo Jumatatu Juni 12,2023.
Afisa ustawi wa jamii wa Halmashauri
ya Manispaa ya Shinyanga Bi. Ansila Materu akitoa elimu ya ukatili kwa
wanafunzi wa timu ya UMISETA Mkoa wa Shinyanga waliopo kambi katika chuo cha ualimu
SHYCOM, leo Jumatatu Juni 12,2023.
Makamu mwenyekiti wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Mwalimu Vicent Kanyogota akitoa elimu ya ukatili kwa wanafunzi wa timu ya UMISETA Mkoa wa Shinyanga waliopo kambi katika chuo cha ualimu SHYCOM, leo Jumatatu Juni 12,2023.
Makamu mwenyekiti wa SMAUJATA Mkoa wa
Shinyanga Mwalimu Vicent Kanyogota akitoa elimu ya ukatili kwa wanafunzi wa
timu ya UMISETA Mkoa wa Shinyanga waliopo kambi katika chuo cha ualimu SHYCOM,
leo Jumatatu Juni 12,2023.
Wanafunzi wa timu ya UMISETA Mkoa wa
Shinyanga ambao wapo kwenye kambi katika chuo cha ualimu SHYCOM wakipata elimu
ya ukatili leo Jumatatu Juni 12,2023.
Mwenyekiti wa kamati ya maadili
SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Bwana Solomon Nalinga Najulwa jina maarufu Cheupe akitoa
elimu kuhusu maadili mema kwa wanafunzi wa timu ya UMISETA Mkoa wa Shinyanga
leo Jumatatu Juni 12,2023.
Mwenyekiti idara ya wanawake SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Bi. Esther Emmanuel akitoa elimu ya ukatili wa kijinsia kwa wanafunzi wa timu ya UMISETA Mkoa wa Shinyanga waliopo kambi katika chuo cha ualimu SHYCOM, leo Jumatatu Juni 12,2023.
Mwenyekiti idara ya wanawake SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Bi. Esther Emmanuel akitoa elimu ya ukatili wa kijinsia kwa wanafunzi wa timu ya UMISETA Mkoa wa Shinyanga waliopo kambi katika chuo cha ualimu SHYCOM, leo Jumatatu Juni 12,2023.
Wanafunzi wa timu ya UMISETA Mkoa wa
Shinyanga ambao wapo kwenye kambi katika chuo cha ualimu SHYCOM wakipata elimu
ya ukatili leo Jumatatu Juni 12,2023.
Wanafunzi wa timu ya UMISETA Mkoa wa
Shinyanga ambao wapo kwenye kambi katika chuo cha ualimu SHYCOM wakipata elimu
ya ukatili leo Jumatatu Juni 12,2023.
Post A Comment: