Mkuu wa mkoa wa Manyara Mheshimiwa Queen Sendiga akisisitiza Jambo katika baraza maalum la Madiwani lililoketi leo Juni 14,2023 mjini Babati.

Mdhibiti na Mkaguzi  Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG)  Charles Kichere akizungumza jambo katika baraza maalum la madiwani Halmashauri ya mji wa Babati mkoani Manyara leo Juni 14,2023.

Na John Walter-Manyara

Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga, amemuagiza Katibu tawala Mkoa kuzipitia Halmashauri zote za mkoa wa huo zenye hati zenye mashaka zilizoorodhedhwa na CAG, kufanyiwa Ukaguzi maalum pamoja na kupitia Mikataba yote upya.

Ametoa agizo hilo leo Juni 14,2023 katika kikao maalum Cha baraza la Madiwani lililolenga kupitia na kujadili hoja 35 za Mdhibiti na Mkaguzi  Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) zilizotajwa katika Halmashauri ya Mji wa Babati yenye hati ya Mashaka.

"Ukaguzi wa maana hapa halmashauri ya mji wa Babati ni muhimu kwa sababu mikataba mingi ina utata" alisisitiza Sendiga

Mdhibiti na Mkaguzi  Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG)  Charles Kichere amepigilia msumari agizo hilo na kueleza kuwa Ukaguzi utakaofanyika ni uchunguzi wa Ukaguzi, watafanya kwa kina kubaini kila kitu na wote wanaohusika kufanya madudu na hatua stahiki zitachukuliwa.
Amewataka Wataalamu haswa wahasibu kutoa ushirikiano pindi wakaguzi wanapopita katika maeneo yao.

"Kuna mambo mengi sana, na sijaja hapa kwa bahati mbaya, Mimi sio Mwanasiasa, lazima tuisaidie halmashauri hii" alisema Kichere

Mbunge wa Babati Mjini Paulina Gekul ameshauri wawekezaji wanaofika kuwekeza ,waripoti ofisi za Halmashauri badala ya kumalizana na Wananchi ili kuepusha migongano.

Ni mwendelezo wa vikao vya kujadili hoja za CAG ambapo mkuu wa mkoa Queen Sendiga  ameshapita Kiteto, Simanjiro na Babati Mjini.


Share To:

Post A Comment: