Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. John Mongela amepokea Mwenge wa Uhuru 2023, kutoka kwa Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu

Mwenge huo wa  Uhuru 2023, umepokelewamapema leo kwenye viwanja vya shule ya Sekondari Tingatinga  wilaya ya Longido, tayari kwa kukimbizwa kwenye wilaya sita na halmashauri saba za mkoa wa Arusha.

Mwaka 2023 Mwenge wa Uhuru mkoani Arusha utakimbizwa umbali wa Km 1,168.47 na kupitia jumla ya miradi 62 yenye thamani ya shilingi bilioni 47.3.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndugu Abdalla Shaib Kaim akiwa mkoani atafanya shughuli mbalimbalo kikiwa ni pamoja na kuweka mawe ya Msingi kwenue miradi 16,  atazindua miradi 12 atafungua  miradi 8 pamoja na kukagua na kutembelea  jumla ya miradi 24 katika sekta ya elimu afya,  maji, mazingira, uwekezaji, miundombinu ya barabara na ujasiriamali.

Aidha kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 atazungumza na wananchi na kutoa jumbe mbalimbali za Mwenge wa Uhuru

KAULI MBIU: " TUNZA MAZINGIRA, OKOA VYANZO VYA MAJI KWA USTAWI WA VIUMBE HAI KWA UCHUMI WA TAIFA"

Share To:

Post A Comment: